Mkutano wa CHADEMA Tandahimba mapema mwezi Juni mwaka huu (Picha ya Maktaba)
Na Andrew Chale
VUGUVUGU la Mabadiliko (M4C) linaloendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limeendelea kuimaliza na kukichanganya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilayani Newala, na kufanikiwa kuzoa wanachama 276.
Katibu wa Chadema, Wilaya Newala, Mhunzi Rashid , katika taarifa yake aliyotolewa jana kwa vyombo vya Habari, ambapo alisema kwa kufanya mikutano ya ukombozi kwenye Kata tano na vijiji vyake vipatavyo 32, wananchi mbalimbali wengi wao wakitokea CCM, walifanikiwa kujiunga na chama hicho.
“Tumetumia uwezo na elimu bora tulioipata kutoka kwa viongozi wa Kitaifa wa Chadema waliopata kutembelea Mikoa ya kusini na pia walipofanya mikutano yao hapa imetutia ujasiri mkubwa nasi na kufanikiwa kupata wanachama hawa” alisema Mhunzi.
Katika mikutano hiyo, Kata ya Kitangari waliwema kambi kwa siku saba kwenye Tarafaa ya Kitangari na kufanya mikutano ya hadhara na kuvunja ngome ya CCM.
Mhunzi alitaja Kata nyingine walizotembea kuwa ni Mtopwa, Maputi, Nandwahi na Chiwonga, ambapo jimbo hilo la Newala lina Kata 28.
Aidha, alitaja baadhi ya vigogo ndanai ya vijiji waliojivua gamba ni pamoja na Mwenyekiti wa kitongiji cha Azimio, akiwemo na Mwenyekiti wa kijiji cha Samora, aliefahamika kwa jina la Mzee Mpotto nae aliamua kujivua gamba na kujiunga Chadema.
Hata hivyo, Mhunzio alisema kuwa katika tathimini yao walibaini kuwa viongozi wengi hawafanyi mikutano ya kijiji na vitongoji kwa wananchi wao kusababisha wananchi kukosa imani na serikali yao iliyochini ya CCM.
0 maoni:
Post a Comment