Waziri Mkuu Pinda amemaliza kusoma hotuba yake ya Hoja ya Kuahirisha Bunge maalumu kujadili na kuidhinisha makadirio ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13 jioni hii. Wabunge watakutana tena 30 Oktoba, 2012.
Hiki kilikuwa ni Kikao cha 49 Bunge la 8 na Pinda alianza kusoma hotuba yake saa moja na nusu jioni hii mara tu baada ya wabunge kurejea kutoka kufuturu.
Pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu amezunumzia mfululizo wa ajali zilizofuluiza nchini katika kipindi hiki Bunge likiwa linaendelea na vikao vyake mjini Dodoma. Ajali ya meli huko Zanzibar na ajali kadhaa za barabarani zilizotokea hivi karibuni. Pinda amewapa pole waliopatwa na madhara kutokana na ajali izo.
Amekumbushia vipaumbele vya Serikali katika bajeti hii kuwa ni Sekta ya miundombinu; nishati, usafirishaji na maji.
Vipaumbele vingine ni Kilimo na ufugaji kwa ajili ya chakula na biashara, Sekat ya viwanda hasa vinavyotumia malighafi inayozalishwa nchini ili kutoa soko la bidhaa za kilimo na kuongeza tamani ya madini, na pia kuvutia uwekezaji katika teknolojia.
Pinda alitaja kipaumbele cha nne kuwa ni kukuza sekta ya rasilimali watu na ujuzi, na mwisho ni kukuza sekta ya utalii, biashara na fedha, vitu ambavyo vitasaidia ukuaji wa uchumi.
Mambo mengine aliyogusia ni pamoja na mchakato wa Katiba mpya, ukosefu wa ajira, afya na sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika ncini kote 26 August 2012.
Makinda aiongezea muda Kamati ya Maadili ya Bunge
Nae Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Makinda ameiongezea muda zaidi Kamati ya Maadili ya Bunge kukalimisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowahusu baadhi ya wabunge.
Hata hivyo, Makinda amewataka wabunge kutoenda kuyajadili maswala yanayohusu kadhia hiyo majimboni kwao ili kutovuruga mwenendo wa uchunguzi.
0 maoni:
Post a Comment