Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Katibu Kata atuhumiwa kwa utapeli

Katibu wa Kata ya Enduleni Wilayani Ngorongoro (CHADEMA), Denis Paulo mwenye umri wa miaka 33 amekamatwa na Jeshi la Polisi Arusha kwa madai ya kutaka kufanya utapeli kwa wafanyakazi wawili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro shilingi mil 16.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amethibitisha kukamatwa kwa Katibu huyo na kueleza kuwa Denis aliwapigia simu wafanyakazi wawili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro NCAA Agosti 27 saa sita mchana kwa nia ya kuwatapeli.

Kamanda Sabas alidai kwamba baada ya kupiga simu kwa wafanyakazi hao, Denis alijitambulisha kwa jina la David Kagasheki na kudai kuwa ni katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa na Habari Leo  toleo la Agosti 31, 2012, ilidaiwa na Kamanda Sabas kuwa Denis alijitambulisha kuwa anatoka tume maalumu ilioungwa na Waziri Kagasheki kuchunguza kashfa mbalimbali katika mamlaka hiyo, na kudai kwamba yeye kama Mwenyekiti wa tume hiyo na wenzake sita, wangewahoji watumishi wa Menejiment ya NCAA na hivyo alidaiwa kuomba shilingi mil 16 ili awasaidie kuzima sakata hilo.

Simulizi ya mtuhumiwa

Blog hii ilipata nafasi ya kuzungumza na mtuhumiwa huyo akiwa kizuizini Kituo Kikuu cha Polisi Arusha jioni ya August 29, 2012 ambako amefunguliwa jalada kwa kosa la kujifanya  mtumishi wa mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo yake, Denis anadai kuwa haelewi kinachoendelea dhidi yake na anahisi  pengine ni njama za makusudi dhidi yake na chama chake kwasababu kwa muda mrefu amekuwa akipata vitisho kutokana na kudaiwa kuvujisha siri za ufisadi wa watumishi wa mamlaka hiyo kwa wabunge wa Wilaya hiyo.

Paulo anasema kwamba siku ya kukamatwa kwake alikuwa anatoka hospitali ya AICC kufuatilia matibabu ya mguu wake ambao aliumia kwenye ajali ya gari siku kadhaa nyuma, na kwamba siku hiyo alipigiwa simu na mtu anaemfahamu siku nyingi aliemtambulisha kwa jina la Vero, mtumishi mwenye cheo kikubwa katika mamlaka hiyo na kwamba amekuwa akipata vibali mbalimbali vya shughuli zake toka kwa mama huyo.

Akisimulia zaidi, Denis anasema, huyo Vero alimtafuta kwa siku tatu mfululizo akimtaka wakutane kwa maongezi fulani na ndipo siku ya kukamatwa kwake wakakubaliana wakutane Hotel ya Palace Arusha iliyoko jirani na osifi za manispaa.

Baada ya kufika hotelini hapo, Denis anasimulia kuwa, alipigiwa simu na mtu mwingine mwanamke asiyemfahamu akiwa eneo hilo na kumueleza kuwa ametumwa amkabidhi mkoba. Akiwa bado anashangaana na mwanadada huyo asiyemfahamu, Densia anasema ghafla walijitokeza watu wengine waliomweka chini ya ulinzi na kumnyang’anya simu zake zote hapo hapo. Mwenyewe anasema alikuwa na simu mbili moja haikuwa na SIM card ndani, na hata alipotaka wampatie awasiliane na ndugu zake kuwaeleza kuwa amekamatwa walimkatalia.

Baadae watu hao wakampeleka Polisi makao makuu wakiwa wameambatana na huyo aliemtambulisha kama Vero na maofisa wengine wa Polisi wakimlazimisha awatajie ni nani aliempatia nyaraka hizo za siri anazodaiwa kuzitoa kwa wabunge Cecilia Pareso ( viti maalumu CHADEMA) na Ole Telele (CCM – Ngorongoro) zikihusu ufisadi wa kutisha ndani ya mamlaka hiyo.

Uchunguzi mdogo wa Blog hii umebaini sehemu kubwa ya kisa hiki inahusu nyaraka fulani za siri za ufisadi ambazo zimevuja nje ya mamlaka hiyo na kuwafikia wanasiasa na mtu anaedhaniwa kuwa ndie aliezivujisha ndie huyo Denis Paulo.

Kwa sasa Densi bado anshikilishwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na taratibu za kulifikisha shauri lake Mahakamani zinaendelea.

Blog hii iliwasiliana na viongozi wa Chadema Mkoani Arusha na kubahatika kumpata Katibu wa chama hicho Mkoa, Amani Golugwa ambae alithibitisha kuwako kwa tuhuma hizo dhidi ya Denis Paulo na kueleza kushangazwa na madai hayo lakini akaahidi kulifuatilia swala hilo kwa kina zaidi.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO