Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CCM KUKATA RUFANI KUTENGULIWA USHINDI WA MBUNGE WA IGUNGA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora.

Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter Kafumu.

Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo.

Imetolewa na;-

Nape Nnauye

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM WA

ITIKADI NA UENEZI

22/08/2012
*******************************************

Taarifa ya awali mapema leo ikiandikwa na BASHIR NKOROMO ilieleza kuwa CCM ilikusudia kukatia rufaa hukumu iliyotengua Ubunge wa Dr Kafumu jana….

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga, Peter Dalally Kafumu.

Taarifa iliyolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye mchana leo, imeseme kufuatia kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Mary Shangali,  kitakata rufani.

"Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora. Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter

Kafumu.Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo". imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Nape.

Jana Jaji  Mary Shangali katika hukumu yake, alisema ametengua ushindi wa Dk. Kafumu baada ya kurishishwa na madai saba kati ya 17 yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo na Mlalamilikaji, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Chadema, Joseph Kashindye.

Dk. Kafumu wa CCM alitangazwa kushinda kiti na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Igunga, katika uchaguzi mdogo uliofanyika, Septemba mwaka jana, baada ya kujiuzulu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Rostam Aziz.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO