Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Ngoma Africa Band kutingisha Jukwaa ALAFIA Festival ,Mjini Hamburg,Ujerumani

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU watatingisha jukwaa la ALAFIA Festival,mjini Hamburg,Ujerumani siku ya jumapili 26.8.2012 ,onyesho hilo kubwa la wazi linafanyika katikati ya kitovu cha mji wa Hamburg, eneo la Hamburg-Altona, ambapo patakua na pata shika ya nguo kuchanika.

Ngoma Africa band inashikilia award ya kimataifa " IDA-International Diaspora Award" kwa kuchaguliwa kuwa bendi bora ya kiafrika inayowakilisha vizuri kimataifa na kuwanasa mamilioni ya washabiki kila kona duniani,imetajwa mara nyingi kuwa bendi bora katika  maonyesho mengi ya kimataifa.

Kikosi kazi hicho kinachoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras makunja wa FFU,kwa sasa kinatamba na CD mpaya "Bongo Tambarare" ambayo inasikika katika kambi yao at www.ngoma-africa.com

kamanda Ras makunja na Award IDA.

FFU wa Ngoma Africa Band na TUZO za Kimataifa.

Ngoma Africa Band" aka FFU

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO