Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

GADNER G. HABASH AHAMIA RADIO TIMES 100.5 FM, KURINDIMA NA KIPINDI KIPYA CHA “MASKANI”

Kapten Gadner Habash ambaye amejiunga na kituo hicho cha redio na kutangazia umma rasmi akizungumza na wanahabari pamoja na watangazaji wenzake, wanaofuatia katika picha ni Scholastica Mazula, Criford Ndimbo na Dida wa Mchops.

Mtangazaji wa Radio Times 100.5 Scholastica Mazula akizungumza na waandishi wa habari kwenye magahawa wa City Sports Lounge Posta jijini Dar es salaam wakato alipomtambulisha rasmi Kapten Gadner Habash ambaye amejiunga na kituo hicho cha redio hiyo. Hivi karibuni atakuja na kipindi kipya kinachokewanda kwa jina la “Maskani” kitakachozungumzia mambo mbalimbali katika jamii, katika picha kushoto ni Gadner G. Habash mwenyewe na kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha michezo Cliford Ndimbo.

Baadhi ya watayarishaji wa vipindi na watangazaji katika redio hiyo watatu kutoka kulia ni mkoloni aliyewahi kuvuma na kundi la Wagosi wa Kaya.

Kapten Gadner Habash kushoto akipozi kwa picha wa mastaafu wenzake wapya kutoka kulia ni Dida wa Mchops, Natasha na Scholastica Mazula

SOURCE: HAKI NGOWI

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO