Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Uchaguzi UVCCM Moshi ni hujuma tupu, kada wa CCM aswekwa mahabusu na kunyimwa dhamana ili asishiriki usaili wa wagombea

uronuMchakato wa uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM kwa Mkoa wa Kilimanjaro umeingia katika dosari baada ya baadhi ya wagombea kutoa malalamiko ya kufanyiwa hujuma za makusudi ili wasiweze kushiriki katika uchaguzi wa umoja huo  unazotarajiwa kufanyika kati ya August 28 na 30 mwaka huu.

Mmoja wa walioathirika na mikakati hiyo ya kubagua wagombea wasiotakiwa na kundi fulani linaloonekana kukamia kuweka watu wao ni kijana Uronu Tumaini (pichani) ambae hapo awali amewahi kuwa kiongozi wa Umoja wa Vyuo Vikuu kupitia chama hicho katika Mkoa wa Kilimajaro kwa vipindi tofauti.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika, inaelezwa kuwa Uronu alitengenezewa kesi na kuwekwa mahabusu tangu Jumatano ya wiki hii na kunyimwa dhamana na kisha kuachiwa leo hii, ikiwa tayari usaili wa wagombea umemalizika.

Urunu akiwa miongoni mwa vijana waliochukua fomu za kuombea na fasi ya Mwenyekiti wa Umoja huo kwa Mkoa wa Kilimajaro na kurejesha mapema mwezi huu,  inaelezwa kuwa ndie pekee alieonekana kuwa na uungwaji mkono na wajumbe wengi kiasi cha kutishia nafasi za wagombea wengine ambao wanapigiwa chapuo na baadhi ya wakongwe wa chama hico kwa sababu ambazo hazijaweza kujulikana.

Kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa, inaelezwa kuwa Uronu ambae kitaaluma ni famasia KCMC, amesikitiswa sana na mchezo mchafu aliofanyiwa kwa makusudi ya kumkosesha nafasi kugombea Uenyekiti wa Umoja huo na ameahidi kutoa tamko kesho kwa waandishi wa habari la ama kuridhia hujuma hiyo au kuamua  kukihama chama hicho endapo atajigundua kuwa hahitajiki katika umoja uo.

Mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu, umoja huo ulitangaza kuanza chaguzi za viongozi wa chama hicho, ngazi ya taifa. Katika chaguzi hizo nafasi mbalimbali zitagombewa ikiwa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti wa umoja huo taifa, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa nafasi sita kwa Tanzania Bara na nafasi nne kwa visiwani. Nafasi nyingine ni Wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, nafasi tano kwa Tanzania Bara na nafasi tano kwa visiwani pamoja na mjumbe mmoja wa kuwakilisha UVCCM katika vikao vya Jumuiya ya Wanawake (UWT) na Wazazi.

Katibu Mkuu wa UVCCM,  Martine Shigela  akitangaza sifa za wagombea siku hiyo alisema kuwa mwombaji wa nafasi hizo za uongozi anatakiwa awe mwanachama hai wa UVCCM  na CCM na anayetimiza haki, wajibu na masharti ya uanachama ikiwa ni pamoja na kuwa Raia wa Tanzania, mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na asizidi miaka 30. 

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO