Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Rais Zuma atangaza maombolezo Afrika Kusini kufuatia vifo vya wachimba madini 34

Baadhi ya miili ya wachimba migodi waliouawa na polisi Afrika Kusini

Baadhi ya miili ya wachimba migodi waliouawa na polisi Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kipindi cha maombolezo nchini humo kufuatia mauaji ya wachimba madini thelathini na wanne yaliyofanywa na polisi, wakati walipokuwa wakiandamana kudai malipo bora zaidi ya kazi.

Bwana Zuma pia ametaka tume ya uchunguzi ya kisheria ichunguze mauaji hayo katika mgodi wa madini meupe yaani PLATINUM eneo la Marikana.

Wakati huohuo wachimba madini wameamriwa kurejea kazini siku ya Jumatatu la sivyo watafukuzwa kazi.

Lakini wengi wamesema kumaliza mgomo wao sasa ni sawa na kuwadhalilisha wenzao waliouawa.

Wanasema watarejea kugoma katika eneo la mgodi huo na wataendelea kushinikiza malipo bora zaidi ya kazi.

Hata hivyo chama cha wafanyakazi wa migodi cha NUM ambacho kina uhusiano wa karibu na chama tawala cha ANC - kinasema wanachama wake wamekubali kurejea kazini.

Mmoja wa wachimba madini hao Vuyisile Mchiza, amesema atarejea kazini iwapo idadi kubwa ya wenzake watakubaliana kusitisha mgomo.

''Iwapo idadi kubwa watarejea kazini kesho, basi na mimi nitakwenda''. Anasema. ''Iwapo wengi hawatakwenda kazini, nami pia sitakwenda, kwasababu sitaweza kufanya kazi wakati wengine wakiwa bado wanaomboleza''. Ameongeza.

Source: BBC Swahili, 19 August 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO