Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mkutano Wa CHADEMA Reading

Ili kufikia malengo yetu ya kuzunguka kwenye Miji mbalimbali ya UK kuhamasisha Watanzania waishio uk kujiunga na Chadema, kueneza kampeni ya m4c na  kufungua matawi mengine, Tawi la Chadema London linapenda kuwatangazia Watanzania wote waishio katika Mji wa Reading na maeneo ya jirani kuwa kutakuwa na mkutano mkubwa wa M4C UK utakao fanyika Tarehe 26/08/2012 siku ya Bank holiday.

Dhumuni  la mkutano huo ni kuwahamasisha Watanzania waishio UK kujiunga na chama, kushiriki katika harakati za mabadiliko, kusajili wanachama wapya, kuchagua  wawakilishi wa muda kutoka mji wa Reading pamoja na kuanzisha mfuko wa kufa na kuzikana kwa manufaa ya watanzania wote.

Tumekusudia kuanzisha Mfuko wa kufa na kuzikana kwa sababu mpaka hivi sasa Mtanzania akifariki akiwa  UK hakuna taasisi wala ofisi yoyote inayotoa msaada. Jukumu ambalo kwa muda mrefu Serikali yetu kupitia ubalozi wamelipuuzia na kushindwa kulishughulikia na kulisimamia.

Mfuko huu utasaidia katika kumsafirisha Marahemu na Mfiwa pamoja na kusaidia kushughulikia matatizo na usumbufu utakaojitokeza  baada ya mtu kufariki dunia na kusaidia matatizo mbalimbali yakiwemo majanga ya dharura.

Pia katika mkutano huo wanachama mbalimbali wa CCM walio na uchungu na nchi yetu na wanaopenda mabadiliko ya kweli watapewa nafasi ya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama sehemu moja wapo ya  kampeni yetu ya Kuvua Gamba na Kuvaa Gwanda ukiwa Ughaibuni.

Mkutano utafanyika siku ya Tarehe 26/08/2012 kuanzia saa saba mchana mpaka saa kumi na mbili jioni, siku ya Bank Holiday. .Risc Reading International Solidarity Centre, 35-39 London Street, Reading, RG1 4PS .

Watanzania wote na wadau mbali mbali mnakaribishwa 

SISI SOTE NI NDUGU, TATIZO NI CCM

ni wakati wa kusimama na kusema tumechoka

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA HAWA WAFUATAO

MWENYEKITI: Chris Lukosi 07903828119

KATIBU MWENEZI:  Chris Chagula 07405889880

Au tutumie email kupitia chademauk@gmail.com

 

HATULALI MPAKA KIELEWEKE!!!!!!!!!!!
Peooooople's Power

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO