Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA:VIONGOZI WA CHADEMA WASHIRIKI SIKUKUU YA IDD NA WAKAZI WA MKOA WA MOROGORO

Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakishiriki katika chakula cha mchana kilichoandaliwa na wenyeji wao wa mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya kuuadhimisha sikuu ya Idd el Fitr, baada ya kusitisha Opereshini Sangara jana ili kuungana na waislamuu nchini kote kuadhimisha sikukuu hiyo. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, mwanachama Arcado Ntagazwa, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed na Mwenyekiti wa Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk.

Viongozi wa Chama cha Demokarsia na Maendeleo (Chadema), wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe (wa nne kutoka kushoto), wakishiriki chakula kilichoandaliwa na wenyeji wao mjini Morogoro, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya Idd el Fitr, baada ya kusitizsha kampeni za Operesheni Sangara katika mkoa wa Morogoro jana, ili kuungana na waislamu kote nchini kusherehekea sikukuu hiyo. Kutoka kushoto ni mwanachma wa chama hicho, Arcado Ntagazwa, Katibu Mkuu, Willibrod Slaa, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed.

************************************

Viongozi wa wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, juzi walilazimika kusimamisha ziara za vuvugu la mabadiliko (M4C) katika Operesheni Sangara wilayani Mvomero ili kushiriki na wananchi chakula cha sikukuu ya Eid El Fitri.

Aidha, Mbowe alitumia muda huo kuwaaga viongozi wenzake pamoja na makamanda wanaoshiriki operesheni hiyo mkoani Morogoro huku akieleza kuwa anatarajia kwenda Florida, Marekani wiki hii kwa shughuli za kuimarisha chama.

Mbowe aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Yusuph Mohamed, viongozi na makamanda wa chama hicho walioko Morogoro kwa shughuli za operesheni ya vuguvugu la mabadiliko.
Wote walishiriki chakula hicho katika mtaa wa Konga Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na wananchi baada ya chakula hicho, Mbowe aliwashukuru makamanda wa chama hicho kwa kushiriki vema katika kampeni za M4C mkoani humu na kueleza kuwa shughuli za ukombozi zinahitaji watu wenye moyo na kujituma.

"Nawapongeza sana makamanda kwa kazi mnayoifanya hapa Morogoro napenda kuwaongezea chachu katika harakati za ukombozi wa mkoa wa Morogoro ambao umeangukia mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi,” alisema.

Alisema baada ya kumalizika kwa sikukuu ya Eid, wabunge wa Chadema wataungana na operesheni hiyo kwa awamu na kwamba kwa sasa wabunge hao wamerejea majimboni kwao kwa muda baada ya Bunge la Bajeti kumalizika.

Alisema baadhi ya wabunge sita wataungana na operesheni ya M4C mkoani Morogoro na wengine wataungana na timu ya operesheni mkoani Iringa ikiwa ni pamoja na yeye mwenyewe.

Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni na Mbunge wa Hai,  alisema chama chake kimejipanga kufanya mkutano mkubwa katika Jimbo la Morogoro na viongozi wote wa chama hicho watashiriki.

Aliwataka wakazi wa mkoa wa Morogoro kutoa ushirikiano kwa timu ya operesheni chini ya mkuu wa operesheni hiyo, Benson Kigaila, ili kuwezesha dhamira ya chama hicho ya kuwawezesha wananchi wa mkoa huu kubadilika na hatimaye kuona umuhimu wa kukichagua chama hicho katika uchaguzi ujao.

Source: HakiNgowi.Com na Nipashe; Picha na Joseph Senga

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO