Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mwanachadema aeleza siri ya mauaji yaliyotokea Morogoro kwenye kufunga Operesheni Sangara mkoani humo leo

Tunalaani vikali mauaji yaliyofanywa leo na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro katika harakati za kuzuia Maandamano ya amani ya CHADEMA. Ikumbukwe kuwa tulitaka kuzindua Operesheni Sangara tarehe 08/08/2012 Morogoro Mjini, RPC akakataa kwa sababu ya sherehe za nane. Baada ya majidiliano ya viungozi wetu Wakuu na IGP tulikubaliana kwenda kuzindua Operesheni yetu Jimbo la Kilombero-Ifakara kwa makubaliano kuwa tutafungia Operesheni yetu Morogoro Mjini kwa maandamano.

Tulipotaka kufunga jana tarehe 26/08/2012 busara ikatushauri tupishe zoezi la sensa na tufunge tarehe 27/08/2012 na tukakubaliana na RPC hivyo tarehe 25/08/2012. Jana jioni ndio RPC anakataa kusiwe na maandamano na badala yake viongozi ndio wawe kwenye msafara wa magari kwani eti shughuli za Morogoro zitasimama. Alipokumbushwa makubaliano akawa na kiburi cha Madaraka.

Leo asubuhi wakati watu wanakusanyika ili wajue namna ya kufanya ndipo Polisi wakaanza kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za Moto hadi kuuwa raia. MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU ALLY ZONA PEPONI. DAMU YAKO HAIJAMWAGIKA BURE KAMANDA ITAKUWA SABABU YA UKOMBOZI WA TAIFA HILI

PANTALEO ANSELEM

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO