Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Breakibg News: Mnyika - Kama Nape amekataa kuomba radhi, CHADEMA kitamburuza Mahakamni


Leo Nape Nnauye amekwepa kujibu hoja ameibua vioja. Kwa kuwa amekataa kuomba radhi, CHADEMA kitamburuza mahakamani kwani madai yake ya uongo kwa CHADEMA imepata mabilioni toka nje hayawezi kuwa na ushahidi wa ukweli.
Nape na CCM wajibu hoja kwa kuwa Dr. Slaa alitaja mpaka namba ya silaha, CCM ilipaswa kueleza iliingiaje nchini na suala ambalo Nape hajui kwa hiyo tunasubiri jibu la Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete. CCM huwa wanatoa madai ya uongo dhidi ya CHADEMA ushahidi ni hukumu ya kesi ya Igunga ambapo ilithibitika Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alizusha kuwa CHADEMA imeingiza magaidi toka nje ya nchi.
Kati ya CHADEMA na CCM ni chama kipi kimepoteza mvuto jibu wanatoa wananchi wanavyounga mkono vuguvugu la mabadiliko (M4C) kwa hali na mali kwa kiwango cha C
CM kufanya siasa chafu.
Baada ya Dr.Slaa kufichua silaha za CCM, leo wametumia za polisi Morogoro. Umma umeweka hofu pembeni, mkutano umejaa nami naelekea huko tukawavue magamba. Peopleeee……..ss!!!
Imeandikwa na
John John Mnyika
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
27 Agosti, 2012
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO