Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye Abwagwa na Dk. Nagu Ujumbe wa NEC Wilaya ya Hanang

 

*Alazimika kuondoka ukumbini kimya kimya bila kuaga

*Wapambe wake wamlalamikia Nagu, watishia kuhama

AMINI usiamini, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, amepigwa mweleka. Sumaye amepigwa mweleka katika uchaguzi wa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kupitia Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara.

Aliyeibuka mshindi katika nafasi hiyo ni Mbunge wa Hanang ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, aliyekuwa akipambana na Sumaye.

Kukamilika kwa uchaguzi huo mkoani Manyara, hasa hasa Wilaya ya Hanang, kumeonekana kuwaacha watu vinywa wazi, baada ya wapiga kura kumtosa Sumaye, aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda nafasi hiyo.

Uchaguzi huo uliokuwa ukifuatiliwa na watu wengi kutokana na kuibua makundi na mivutano ya wapambe, ulihitimishwa kwa wapiga kura 1,150 kushiriki uchaguzi huo.

Katika uchaguzi huo, Dk. Nagu aliibuka mshindi kwa kupata kura 648, huku mpinzani wake (Sumaye) akiambulia kura 481. Kura 41 ziliharibika.

Hata hivyo, mgombea mwingine katika nafasi hiyo ya NEC kupitia Wilaya ya Hanang, Leons Marmo, aliamua kujitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa hiari yake.

Uchaguzi huo ulikamilika jana saa 10 alfajiri na ulikuwa ukisimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo.

Baada ya Mbwiro kumtangaza Dk. Nagu kuwa ndiye mshindi, wafuasi wa Sumaye walijikuta wakiondoka eneo la tukio kwa hasira wakionyesha kutoamini kilichotokea.

Chanzo cha habari hizi kilichokuwa ndani ya ukumbi huo kilisema kuwa, baada ya Dk. Nagu kutangazwa mshindi, wafuasi wa Sumaye walianza kutishia kuihama CCM, huku wakimtuhumu Dk. Nagu, kwamba alitumia fedha nyingi kufanikisha ushindi huo.

“Ndugu yangu, kundi la Sumaye liligoma kabisa kumpongeza Dk. Nagu hadi pale Msimamizi wa Uchaguzi alipowaomba wakubali matokeo ili kuimarisha uhai wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Pamoja na wafuasi hao wa Sumaye kuonyesha kutoridhishwa na matokeo, pia Sumaye alipoona kuna kila dalili za yeye kugaragazwa, aliondoka ukumbini kimya kimya hata kabla ya matokeo kutangazwa,” kilisema chanzo hicho.

Katibu wa CCM, Mkoa wa Manyara, Ndekubali Ndeng’aso, aliiambia MTANZANIA kwa simu jana, kwamba uchaguzi huo mkoani Manyara ulimalizika kwa amani katika wilaya nne, huku wilaya mbili zikitarajia kuchaguana leo.

“Hatukuwa na malalamiko rasmi ya rushwa kutoka kwa wagombea, lakini pia tulijipanga vizuri kuhakikisha vyombo vya usalama vinakuwapo na maofisa wa TAKUKURU walifuatilia kwa karibu sana uchaguzi huu,” alisema Ndeng’aso.

Aliwataja wagombea wengine walioshinda katika wilaya nyingine kuwa ni pamoja na Wilaya ya Hanang kwa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ambapo Michael Bayo alishinda kwa kura 647 dhidi ya Goma Gwaltu aliyepata kura 162 na Hassan Hilbagiloy aliyepata kura 291.

Habari zaidi KONG’OLI HAPA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO