James Ole Millya akilakiwa na wananchi wakati anawasili eneo la mkutano, jirani na ofisi ya CCM ya Kijiji cha Magadirisho kilichopo eneo la Usa-River Wilayani Arumeru.
Katibu wa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Ndg Toti Ndone, ambae pia ni Katibu wa Cama Wilaya, akifafanua masuala mbali mbali ya kiutendaji na kuainisha juhudi za Mbunge huyo kijana zilizofanyika hadi sasa katika kushugulikia maswala ya ardhi, maji, na swala la ajira kwa vijna na kina mama na aadi nyingine alizozitoa wakati wa kampeni. Ndondi alisema Usajili wa Shirika la Maendelo la Jimbo umekamilika na kwamba mwakani litaanza kusomesha watoto waishio kwenye mazingira magumu kiucumi. Pia akaelezea ziara ya Mbunge Nassari kwa Jimbo zima kuanzia mwezi ujao.
Kwa mujibu wa maelezo ya Katibu huyo, Nassari leo atakagua mradi wa maji eneo la Ngarenanyuki
James Millya akizungumza mkutanoni hapo ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura na kujiandikisha ili waweze kushiriki uchaguzi ujao na kuitoa CCM madarakani kwasababu imesindwa kubadili maisa yao. Alitoa wito pia kwa wananchi hao kushiriki mchakato wa katiba mpya na sensa ya watu na makazi kwa ukamilifu kwasababu ndio dira ya maendeleo.
Akikumbushia kilichomtoa CCM, huku akishangiliwa sana, alisema kuwa awezi kuwa seemu ya watu wasio na damira ya kuwakomboa watanzania kutoka kwenye lindi la umasikini uliokithiri. Akisisitiza zaidi alisema nchi imegeuzwa kuwa ya watu nane tu wanoitafuna kama watakavyo na kuahidi kuwataja majina siku nyingine.
Alisema tofauti anayoiona Chadema tofauti na alipokuwa CCM ni kuwa watu wa CHADEMA wanaupendo sana kwa kila mmoja.
Millya akizungumzia tatizo la ajira kwa vijna alisema vijana hawana matumaini na maisha na ambao wana matumaini ni wale ambao wazazi wao wana madaraka ccm au serikalini. Alitumia nafasi hiyo pia kuponda uteuzi wa MaDC na kulalamika kuwa hakuna hata mzawa mmoja kutoka Arusha alieteuliwa katika uteuzi wa hivi karibuni uliofanywa na Rais Kikwete.
Millya akidondosha kadi za CCM zilizorudishwa
Kadi zinakusanywa kwenye kilemba kilicosalimishwa pia
Hapa Millya akigawa kadi kwa wanachama wapya
Millya akipita kukusanya michango ya wananchi kusaidia kazi za chama Waliayani humo, hususani kijijini hapo Magadirisho. Jumla ya Sh 195,550 zilipatikana
Wengine wakichangia kwa njia za mitandao
Makamanda wa chama hicho kutoka Arusha mjini wakishangaa namna ya utumaji michango kwa njia ya mitandao jinsi inavyofanya kazi
Millya akipokea wanachama wapya jukwaani
Watu wa bodaboda wakaweka kambi mbele ya Ofisi ya CCM ya kijijini hapo
0 maoni:
Post a Comment