Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mahakama yawabwaga walimu

*Yaamuru CWT kuilipa Serikali gharama zote
*Yaagiza wanafunzi wafidiwe muda uliopotea
*CWT kutoa tamko rasmi leo kwa waandishi
*HakiElimu yasikitishwa Serikali kukosa fedha

mgomo-stopRais wa Chama cha Walimu Tanania (CWT), Gratian Mukoba akiwa ameambatana na baadhi ya walimu wakati wakitoka Mahakama kuu, kitengo cha kazi jijini Dar es Salaam jana kusikiliza maamuzi ya mahakama hiyo kuhusu kesi yao dhidi ya Serikali. Mahakamama ilisitisha mgomo wa walimu ikidaiwa kuwa ni batili. (Picha na Venance Nestory wa Gazeti Mwananchi)

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi, imekiamuru Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kusitisha mgomo wa walimu nchini mara moja.

Mbali na agizo hilo, Mahakama imeitaka CWT kuilipa Serikali gharama zote na kuwafidia wanafunzi muda uliopotea wakati wote wa mgomo huo.

Uamuzi huo, ulitolewa jana na Jaji Sophia Wambura, alipokuwa akisoma uamuzi uliofikiwa na mahakama, baada ya kupitia hoja zilizowasilishwa na pande mbili zinazopingana.
“Nimepitia na kuzingatia hoja za pande zote mbili, mahakama imeona mgomo ni batili, kwani sheria hazikufuatwa katika kutangaza mgomo.

“CWT walitoa notisi ya saa 48 kuanza mgomo, wakati muda huo ulikuwa wa mapumziko, hivyo mwajiri hakuwa na nafasi ya kujiandaa kulinda mali zake kama sheria inavyotaka,” alisema.

Alisema mgomo ulianza kabla ya saa 48 kutimia, kwani zilitakiwa kuanza kuhesabika kuanzia siku za kazi na kwamba walitangaza wakati upigaji kura ukiendelea, pia hawakueleza utadumu kwa kipindi gani.
“CWT inatakiwa kuilipa Serikali gharama na kuwafidia wanafunzi muda wao waliopoteza kwa kukosa masomo wakati mgomo huo ukiendelea,” alisema Wambura.

Jaji Wambura, alimwamuru aliyetangaza mgomo huo kutangaza kupitia vyombo vya habari kwamba waliogoma wote wanatakiwa kurudi kazini mara moja, mgomo ni batili.
Uamuzi huo, umetokana na maombi ya Serikali ya kusitisha mgomo huo kwa muda kwa sababu ni batili haukufuata sheria.

Wakili wa Serikali, Obadia Kamea, alisema mgomo ulitangazwa wakati upigaji kura ulikuwa haujamalizika na kwamba walitoa notisi siku za mapumziko ambazo kisheria hazihesabiki.

Wakili wa utetezi, Gabrieli Mnyele, alisema mgomo ulikuwa halali, kwani walizingatia taratibu zote kabla ya kufanya hivyo, ikiwemo kutoa notisi ya saa 48 kwa ajili ya kuanza mgomo Julai 30, mwaka huu.

Kuanzia jana saa saba mchana, mahakama ilifurika watu kwa ajili ya kusubiri uamuzi huo ambao ulipaswa kusomwa saa 8. Hata hivyo uamuzi ulisomwa kuanzia saa 9 alasiri.

Pamoja na kushindwa, maofisa na walimu waliofurika mahakamani walitoka huku wakiimba wimbo wa mshikamano ndani ya mahakama

Published by Mtanzania, 3rd August 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO