Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

The Palace Hotel Arusha ilivyoboresha bustani ya manispaa

Kufuatia uwekezaji wa miradi ya hoteli kubwa mjini Arusha, baadhi ya maeneo yamejikuta yakibadilika na kuvutia baada ya kufanyiwa maboresho makubwa na wawekezaji hao.

Ukitembelea zilipo ofizi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuzunguka Mnara wa Mashujaa, utakutana na mandhari nzuri na ya kuvutia ikiwa na sehemu maalumu za kupumzikia.

Muonekano huu mpya wa eneo hili unatokana na ufadhili wa wamiliki wa hotel mpya iliyojengwa eneo hilo “The Palace Hotel Arusha

Dr Hans Macha, Mkurugenzi wa The Palace Hotels Ltd ya Dar es Salaam aliomba kibali Manispaa kupaendeleza kwa gharama zaidi ya mil 120 ili kuweka mandhari nzuri kwa hotel yake iliyo mkabala na eneo hilo.

Itakumbukwa kwamba eneo hilo hapo awali lilikuwa likitumiwa sana na kina dada wanaojiuza na wateja wao kufanya vitendo vya ngono nyakati za usiku.

Kwa sasa ni vigumu kupata nafasi ya kufanya ufuska eneo hilo kwasababu kuna walinzi muda wote na pia kumewekwa taa zinazowaka muda wote nyakati za usiku.

SAM_3383

SAM_3389

SAM_3387

SAM_3507

Hotel ya Palace Arusha kama inavoonekana pichani.. sehemu ya kuingilia mapokezi

Picha & Maelezo: Tumainiel W. Seria

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO