Katika miji mikubwa duniani swala la msongamano wa magari barabarani (traffic jam) ni la kawaida. Kwa mataifa yaliyoendelea wamejaribu kubuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na adha ya foleni.
Hapa kwentu Tanzania, hususani kwa jiji la Dar es Salaam, foleni za barabarani zimekuwa kero kubwa kwa wananchi wengi na watafiti wameweza kuthibitisha kuwepo kwa athari kubwa sana kiuchumi kwa nchi.
Kwa muda mrefu imezoeleka kuwa Dar es Slaama ndio mahali ambapo wakaazi wake wanakosa raha ukifika muda wa kurudi kutoka makazini. Lakini sasa baadhi ya miji mingine nayo inaonekana kukumbwa na kadhia hiyo.
Wakazi wa Jiji la Arusha wameanza kuona kero ya foleni za magari barabarani tofauti na hapo awali. Hali imekuwa ya msongamano zaidi hasa kipindi hiki ambacho kuna ukarabati mkubwa unaendelea mjini hapa wa kuboresha barabara zote kuu za mjini kwa kiwango cha lami. Unafuu pekee unaoonekana ni vile foleni ya Arusha inasogea tofauti na Dar ambako kuna wakati dereva anakwama mahali kiasi cha kulazimika kuzima gari yake kabisa.
Picha hii inaonesha hali halisi ya msongamano barabarani kwa maeneo mengi ya jiji la Arusha hivi sasa.
0 maoni:
Post a Comment