Leo asubuhi mlipuko wa mabomu uliotokea katika kanisa la kikatoliki la Mt Joseph Mfanyakazi – Olasiti Jijini Arusha. nakupelekea vifo na majeruhi kwa baadhi ya waumini waliohudhuria katika sherehe ya uzinduzi wa Parokia katika kanisa hilo, mgeni rasmi akiwa Balozi wa Papa wa Vatican.
Blog hii iliendelea kufuatilia tukio zima na hii ni ripoti ya hadi jioni ya leo…
Chanzo
Kijana huyo(chini pichani aliyevalia tisheti ya njano) ameeleza kwamba bomu hilo lilirushwa na kijana mmoja ambaye kimwonekano alikuwa ni kijana wa kati ya miaka 20-25, na kwamba baada ya kijana huyo kurusha bomu alikimbia kutoka eneo hilo.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa
Kuna kijana ambaye alishirikiana na wananchi wengine kumkimbiza mtuhumiwa kutoka Olasiti mlipuko ulipotokea hadi katika kijiji kiitwacho Ndorobo.
Kijana huyo (mtizame mwisho kabisa katika post hii) alisimulia kuwa mtuhumiwa alikimbia kisha alijilaza katika miwa asionekane ila kwa msaada wa mbwa waliokuwa wakimkimbiza mtuhumiwa huyo walifanikiwa kumkamata na mara baada ya kumkamata walimkuta akiwa na mfuko wenye mabomu yalizobakia.
Muda mfupi baadae wananchi wenye hasira kali walifika eneo alipokamatiwa mtuhumiwa huyo wakiwa na silaha kali za jadi wakitaka kumuua kijana huyo lakini Polisi waliokuwa wakisaidiana na wananchi hao walifika eneo lile nakumchukua mtuhumiwa huyo.
Waliojeruhiwa ni pamoja na Consensia Mbaga(53) Christopher Raymond (10),Deborah Joachim(24) Elizabeth Isdori(24),Anna Didas(52), Bertha Cosinery(49),Edda Ndowo(77) Derick Cyprian(8),Faustine Andrea (35),Mary okech,Neema Daud(13).
Watu wengine ni Mesoit Siriri (33) ,Clenes pius(22),Joyce yohana (15) ,Restuta Alex(50), Mathias Riha (74), Magreth Andrew(45), James Gabriel (16), Regina James (17), Elizabeth Masawe(15), Elizabeth Sauli(18), Njau (35),Yasinta Msafiri (160 na Doreen
Pancras(28). Idadi wajeruhi wengine ni Alex Arnold,Agripina Alex(9),James
Gabriel(16),loveness nelson (17) ,Amalone Pius(25),Frank Donatus (10) ,Alphonce Nyalandu (26),Athanasia Reginald (14),Phillemon Ceressa(49) ,Neema Daud(13)Sophia Kanda(72) ,Theofrida Inocent(21), na Regina Darnes(17).
Hatujaweza kupata jina la mwanakwaya aliyefariki na mtuhumiwa aliyekamatwa kwa sasa…
Dakika chache baada ya mlipuko hivi ndivyo watu walivyodhurika
wananchi wakiwa wameanguka chini huku wengine wakiwa wanakimbia mara baada ya mlipuko kutokea katika kanisa la mtakatifu joseph
hapa maaskofu na balozi wakiwa wanabariki chumvi kabla ya mlipuko kutokea hivi leo
maafisa polisi wakiwa wanachunguza ni bomu la aina gani limetupwa hapo
mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma
sehemu bomu lilipotua
Baadhi ya wananhi waliofika hospitali ya Mt Merru
Kijana aliyeeleza kushuhudia mlipuko ulivyotokea akisimulia hali ilivyokuwa
Tunaomba radhi kwa picha hii! Mmoja wa waliofariki, alikuwa mwanakwaya
Kijana aliyemkimbiza mtuhumiwa akisimuliza jinsi alivyoweza kumkimbiza mtuhumiwa hadi kumkamata.
Jengo la Kanisa Jipya lililokuwa lizinduliwe leo
Askari wakilinda usalama kwenye eneo la tukio Olasiti
Mabaki ya viatu huku Polisi wakianza kuchunguza mlipuko
Padri na Mtawa ambao hawakufahamika majina yao mara moja wakiwa hawaamini kilichotokea
Balozi wa Vatican nchini,Askofu Mkuu Fransis akiondolewa kwenye eneo la Kanisa hilo kwa usalama wake
Balozi wa Vatican hapa nchini,Askofu Mkuu Fransis akiingia kwenye gari kuondoka
Majeruhi
majeruhi mwingine
Mtoto nae alikuwa miongoni mwa walioathirika
Majeruhi alionekana kusaidiwa muda wote
Mama huyu akiugulia maumivu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas akizungumza na waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa mmoja anashikiliwa kwa mahojiano kufuatia tukio hilo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo akizungumzia tukio hilo na hatua za kusaidia majeruhi
Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki wakiwasili eneo la tukio Olasiti
Padri Festus Mangwangi
Wananchi waliojitokeza kushuhudia
Mbunge wa Arumeru Mashariki,Joshua Nassari(kushoto)na Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema wakimfariji majeruhi
Credit: Nyumba ya Habari na Filbert Rweyemamu
0 maoni:
Post a Comment