Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MWENYEKITI WA CCM, RAIS KIKWETE AFANYA KIKAO MUHIMU NA WABUNGE WA CCM LEO MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini wakati wa kikao chake na wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine kushoto ni Spika wa Bunge Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kikao chake na wabunge wa CCM, leo Mei 19, 2013, katika ukumbi wa jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine kushoto ni Spika wa Bunge Anna Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula.

  Wabunge wa CCM wakiwa kwenye kikao chao na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete leo kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Wajumbe kwenye kikao hicho wakibadilishana mawazo ukumbini. Walioketi mbele, Kushoto ni Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakiah Meghji na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migoiro na Mbunge wa Urambo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai na Katibu wa NEC Oganaizesheni Dk. Muhammed Seif Khatib kwenye kikao hicho.

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro(kulia) akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Mbunge wa Same Anne Kilango Malecela.

Mbunge wa Songea na Waziri wa Mambo ya Ndani,Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akitaniana kuhusu Uyanga na Simba na Mwenyekiti wa Simba, Mbunge wa Tabora Aden Rage nje ya ukumbi kabla ya kuanza mkutano huo. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya.

Mbunge wa Bunga Steven Wasira (kulia) akibadulishana mawazo na wabunge wenzake, Dk. Kamani na Mkullo kabla ya kikao kuanza

Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan (kushoto) akibadilishana mawazo na wabunge wenzake Khamis Kagasheki na Shabiby nje ya ukumbi

Wabunge wakifurahia jambo nje ya ukumbi wakati wa mkutano huo, Kutoka kushoto ni Dk. Mary Mwanjelwa,  Ritha Kabati, Angela Kairuki, Beatrice Shelukindo na Vicky Kamata

Shabiby akizungumza na Angela Kairuki

Vicky Kamata na Ana Kilango Malecela ukumbini

Dk. Asha-Rose Migiro akimsalimia Mama Anna Kilango Malecela

Dk Maua Daftari na Samiah Suluhu ukumbini

Job Ndugai akimpongeza Mbunge wa Igunga Dk. Dalaly Peter Kafumu kurejeshewa Ubunge

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimsalimia Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa wakati wa kikao hicho cha Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na wabunge wa CCM

Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe akimsikiliza kwa makini Mbunge mwenzake Innocent Kalogeris  wakati wa mkutano huo. Picha zote na BASHIR NKOROMO

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO