Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Nasaha za Mathias Lyamunda baada ya kuangalia video inayomuonesha Profesa Lipumba akikiri CUF kushiriki kuokoa Jahazi la Kikwete Uchaguzi wa 2010

Si Kawaida yangu kuandika sana ila kwa hili mniwie radhi naandika yafuatayo kwa maslahi ya taifa langu Tanzania:
Baada ya kuangalia VIDEO ya Prof. Lipumba mwenyekiti wa CUF akiwahutubia waislam kwenye Msikiti wa Idrissa, na kutoa rai ya wazi kuwa Waislam wajipange kwa uchaguzi wa 2015 kwasababu wenzetu(Wakristo) wanajipanga, pia wajipange kupigania waislam na wao kuwa raia wa daraja la Kwanza hapa Tanzania. Pia kwa kutamka wazi wazi bila chenga kuwa Waislam Waliokoa Jahazi la CCM/KIKWETE lisizame 2010.
Pamoja na kwamba mimi si mwanachama wa CUF lakini nilikuwa namheshi Lipumba kama Msomi wa taifa hili lakini kwa kauli yake ya wazi kabisa ya kuwataka waislam wamchague ili akapiganie imani kwenye Ikulu ya Taifa hili imenifanya niondoe heshima niliyokuwa nayo kwake, na sasa napenda nitoe rai yangu kwa watanzania wenzangu tunao lipenda taifa hili bila kujali tofauti zetu Imani:
1. Tanzania ni taifa moja la watu wamoja, kamwe haitatokea tanzania ikaongonzwa na itikadi au imani ya kundi moja liwe kundi kubwa au kundi dogo
2. Maadili ya Taifa aliyo yaasisi mwalimu Nyerere hayakuwa kwa ajili ya CHAMA kimoja cha siasa, au kundi la dini flani yalikuwa ni maadili ya taifa lote, kwamba watanzania bila kujali tofauti zetu za kidini, kabila, maeneo tunayotoka, au vyama tukae pamoja kwa upendo na amani.
3. Chama cha Mapinduzi (CCM) kilipaswa kuwa mlezi wa maadili haya lakini kimeshindwa na pia kimehusika katika kuyahujumu haya maadili kwa maslahi yao ya kisiasa
Viongozi wa dini zote hasa wakristo na waislam wanaonekana kuzidiwa na kutekwa kifikra na kiuchumi na makundi ya wasaka urais ambao wamevamia makanisa na misikiti
Hivyo Basi napenda kusema yafuatayo kwa watanzania ambao bado wanaamini katika umoja wa Taifa hili:
1. Tusikubali kugawika kwa maslahi ya kisiasa ya wanasiasa uchwara waliofilisika na kukosa sera za kuwaambia watanzania, wanaanza kutumia makanisa na misikiti kujihalalisha
2. Tukubali wanasiasa watuaminishe kuwa tukiwachagua kwa misingi ya dini zetu eti watatutumikia na kutufanya tuwe wananchi daraja la kwanza, ni nani huyo atakayekubali kuwa daraja na pili, tatu au nne? Huu utakuwa mwanzo wa kuanguka kwa taifa linaloitwa tanzania
3. Chama cha Mapinduzi kimeshindwa kusimamia misingi na maadili ya taifa hili, kimsingi chama hiki ndo kimetufikisha hapa, na kwenye Hotuba ya Lipumba amemtaja mgombea wake wa urais 2010 anawezeshwa na kura za kudi la dini yake ambao sasa wanasema hajaweza kuwatimizia malengo yao ya kuwafanya kuwa raia daraja la kwanza kwenye nchi yao Tanzania. Hiki Chama ndo kinapaswa kuwa adui wa kila mtanzania leo, hiki chama ndo waislam na wakristo wanapaswa kukichukia, maana kimelenga kutugawa watanzania tuchukiane, tuuane kwa tofauti ya dini zetu ili chenyewe kiendelee kutawala.
4. Natoa Rai kwa viongozi wa dini zote, wafukuzeni wanasiasa uchwara waliovamia makanisa na misikiti yenu, taifa hili likianguka nyie hamtaacha kulaumiwa, ni bora taifa hili likaanguka kwa ukabila kuliko likianguka kwa udini, itakuwa ni aibu kubwa kwa viongozi wetu wa dini, acheni kukumbatia viongozi wa serikali wanaotumia madhabahu takatifu kuongea maneno ya hadaa kwa watanzania.
5. Kama hii serikali ya CCM bado ipo madarakani wamkamate mara moja mwenyekiti wa CUF Lipumba kwa uchochezi wa kidini wa wazi wazi.
Natoa wito kwa watanzania wenzangu tuamke, tuchukue hatua, bila hivyo taifa hili limekaribia anguko lake. EEEH MUNGU TUSAIDIE.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO