Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Barua ya Zitto kwa Waziri Kigoda la kuzuia wasanii kunyonywa katika RBT

PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES)

Kwenda kwa:           DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara

Kuhusu:                    BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)

Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania.  Suala la USIRI lipo Wizara  ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.  Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara.

USIRI

Biashara hii ya “Ring Back Tones” (RBT)  hufanywa na Kampuni za simu (Network providers) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao  nao huingia mikataba na Wasanii (Content Creators). Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo “Network providers” na “Content  Providers” kuwa watu pekee wenye taarifa zote za biashara hii.  Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake mengine (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au ‘content’ nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii.  Wachuuzi (Content Providers) nao  hawatoi taarifa za  mauzo kwa wasanii na wanatumia uelewa mdogo wa  wasanii kuwasainisha mikataba inayowanyonya.  Matokeo yake ni kwamba msanii hupata kiasi cha

asilimia mbili tu (2.5%) ya mapato ghafi ya kazi yake.  Hivi sasa biashara hii inathamani (turnover) ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.

Suluhisho:

Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) zitakazolazimisha makampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na biashara ya RBT (Miito ya simu) kila baada ya miezi 4 (disclosure rules).  Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoa taarifa za mauzo kwa kila kazi (nyimbo/vichekesho etc.)

UNYONYAJI

Kutokana na usiri ulioelezwa hapo juu, wasanii  wamekuwa wakinyonywa kimapato.  Kwa mfano Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake (wimbo) katika mwezi (downloads).

Lakini mapato yatokanayo na “subscriptions” ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila siku msanii hapati chochote.  Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mteja kwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za ‘downloads’ na ndio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44 bilioni zinazokusanywa na Kampuni za Simu.

Nchini Marekani biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (Public Performances)  na hivyo “copyright Association”  ya Marekani imeweka kiwango cha chini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa.  Marekani msanii hulipwa asilimia 10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi yake kama muito wa simu.

SULUHISHO

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kazi za wasanii kama miito ya simu inachukuliwa kama ‘performance’ na kwamba Kampuni za simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya  mapato ghafi, ambapo asimilia 10% itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya usimamizi  na Ulinzi wa kazi za Wasanii.

HITIMISHO

Kanuni za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya ‘Ring Back Tones’ na mgawo wa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho endelevu na litakaloleta tija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali kukusanya mapato stahili. Kanuni (Regulations) zinazopendekezwa zianze kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013

Kabwe Z. Zitto, Mb

Kigoma Kaskazini

Dodoma, 13 Mei 2013.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO