Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Lema anogesha kampeni Arusha, Dr Slaa Simanjiro na Mbowe aunguruma Songea

MHESHIMIWA LEMA KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA KALOLENI JIJINI ARUSHA

DSC07052Mzee Singoi akizungumza katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Soweto-Kaloleni jana

 

 

2013-05-26 18.02.17Sehemu ya umati wa wananchi waliojitokeza kuhudhuria mkutano huo wa Chadema jana

DSC07056Katibu wa Chadema Arumeru akisalimia wananchi

2013-05-26 16.06.37Mh Lema aktika jukwa la viongozi wa chama. Katika mkutano huo Mh Lema aliponda utetezi wa Jeshi la Polisi dhidi ya tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kumtumia sms ya vitisho na kuwatupia shutuma Jeshi la Polisi kuwa linafanya kazi ya kuisaidia CCM katika siasa zake.

DSC07054James Milly akifurahia jambo na kiongozi wa Vijana Arumeru Mashariki, Methew Kishili


MHESHIMIWA FREEMAN MBOWE AKIHUTUBIA WAKAZI WA SONGEA

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh Freeman Mbowe akihutubia umamti wa wakazi wa Songea waliojitokeza kusikiliza hotuba za viongozi wa Chadema jana katika uwanja wa Shule ya Msingi Matalawe

Kamanda Antero Assey mwenye kombati za chui chui akihakikisha usalama wa mh Mbowe

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ndugu Freeman Mbowe akizungumza kwenye mkutano uliofanyika katika manispaa ya Songea jana jioni.

Taifa lipo katika kipindi kigumu kutokana na wananchi kukabiliwa na umaskini wa kupindukia unaosababishwa na mfumo uliopo kulenga kuwanufaisha watu wachache wakati walio wengi wanazidi kubaki maskini.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mheshimiwa Freeman Mbowe, alipokuwa akihutumia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Matalawe Manispaa ya Songea.

Mbowe alisema kuwa wananchi wamebaki maskini kiasi kwamba kila sehemu wanalia juu ya hali ngumu ya maisha kutokana na mfumo uliopo kutowasaidia.
Vivile aliwasihi wananchi kuunganisha nguvu bila kujali vyama ili kudai haki zao kitaifa.

“Ndugu wananchi tuache ushabiki wa vyama, wanachadema msigombane na wana-CCM kwa sababu wako CCM na wala uliye katika chama kingine usimchukie aliye Chadema... Mwanachadema ukiona mtu amebaki CCM ujue hujafanya kazi ya kutosha kumuelimisha hivyo unawajibika kumshawishi zaidi ili akuelewe”. Alisema Mbowe.

"Sisi ni watoto wa maskini tunahitaji kuunganisha nguvu  ili kuikomboa nchi hii kutoka mikononi mwa watawala wachache, wasiowajibika, ambao hawalitakii mema taifa letu".

Aidha, Mbowe alitahadharisha juu ya tabia ya serikali kutumia risasi na mabomu bila sababu za msingi kiasi cha kuwafanya wananchi waanze kuiogopa Serikali na kutokuwa na imani nayo.

“Tunajenga Taifa la watu waoga na wasiojiamini tena matokeo yake  wananchi wameacha kumwogopa Mungu wanawaogopa watawala” alisema.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA akizungumzia mfumo wa utawala uliopo, alisema unawapa nguvu zaidi za kimaamuzi viongozi wanaoteuliwa na Rais kuliko wawakilishi halali wa wananchi kwa vile wateule wa Rais hufanya baadhi ya maamuzi mazito kwa nchi ambayo wawakilishi wa wananchi hawayaoni kutokana na usiri uliopo, ambapo alitolea mfano wa mikataba ya Gesi na madini kuwa haiko wazi.

Alisisitiza kuwa kitendo cha kumpa Rais uhuru wa kuamua mtu wa kumchagua kinatoa mwanya kwa Rais kuteua baadhi ya watendaji kwa maslahi binafsi, undugu na hata urafiki jambo linaloifanya serikali ishindwe kuwajibika ipasavyo.

Akaendelea kusema msimamo wa Chadema ni kuona wakuu wa wilaya na mikoa wanachaguliwa na wananchi na wawe wenyeji wa maeneo wanayotaka kuongoza tofauti na sasa ambapo wanaweza kuongoza popote pale nchini.

Akizungumzia suala la mgogoro wa gesi Mtwara, Mbowe alisema serikali haikupaswa kutumia nguvu kubwa ya kuwapiga wananchi kwa mabomu au risasi badala yake ilipaswa kukaa nao ili kupata suluhu ya kudumu.

Awali Kaimu mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi, Ally Omary Chitanda alisema migogoro inayotokea katika nchi hii, ukiwemo wa Mtwara, inasababishwa na serikali ya CCM kutokuwa tayari kuwasikiliza wananchi pamoja na mfumo wake unaowapa mamlaka watu wachache waishio Dar es Salaam kutaka kila kitu kizuri kiwe Dar es Salaam na kuwasahau watu wa mikoani.

Naye mwenyekiti CHADEMA mkoa wa Ruvuma ndugu Edson Mbogoro aliishutumu serikali ya CCM kulitumia jeshi la polisi vibaya na kulifanya lipoteze hadhi yake kisha akalitaka  jeshi la polisi kuwa huru kwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria zinavyotaka

Picha na maelezo: Chadema Blog


Pichani ni Umatiwa watu katika Mkutano wa Dkt. Slaa jana Mirerani, Simanjiro, kuhitimisha siku 9 vijiji vya wilaya za Mkoa wa Manyara

dr slaa simanjiro

KATIBU Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, amesema viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni wanafiki ndiyo maana amani na utulivu vinaanza kupotea.

Alisema serikali ya chama hicho ni mtuhumiwa mkubwa wa uvunjifu wa haki mbalimbali za wananchi lakini imekuwa kinara wa kuzungumzia amani ambayo ni tunda la haki.

Kauli hiyo aliitoa juzi mkoani Manyara alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kukijenga chama ambapo alisema viongozi wa CCM wamekuwa wakihubiri amani bila kuzungumzia haki ambayo ni msingi wa amani na utulivu imara.

“Kama watawala wangekuwa na dhamira ya dhati na amani ya nchi hii, wangetenda haki, amani haihubiriwi majukwaani ni tunda la haki na matumaini ya wananchi kwa viongozi wao,” alisema.

Alisisitiza kuwa ni vigumu kwa viongozi kueleweka kuwa wana nia ya dhati kuona nchi ikitawalika kwa amani na utulivu, wakati wananchi wengi wanaendelea kutaabika kwa kunyimwa haki zao na kunyanyaswa ndani ya maeneo yao.

“Nani hajui uvunjifu wa haki za wananchi unaofanyika katika ardhi, elimu, ajira na usalama wa raia?...haya yanafanywa chini ya serikali ya CCM ambayo inahubiri amani inaacha haki, hawa ni wanafiki ndiyo maana nchi inawashinda,” alisema.

Dk. Slaa pia alisema CHADEMA inajisikia fahari kuona serikali ya sasa inatekeleza sera za chama hicho kikuu cha upinzani nchini chenye utajiri wa mawazo mbadala mbalimbali namna ya kuwatumikia Watanzania.

Alisema wamefurahi kusikia serikali ina mpango wa kuongeza miaka ya wanafunzi kusoma elimu ya msingi kutoka miaka saba ya sasa hadi 10, ambayo ilikuwa sera ya CHADEMA siku nyingi na waliinadi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, akadai kuwa kutokana na mawazo mgando ya chama kilichoko madarakani na viongozi serikalini, walimbeza.

“Tunashukuru wameanza kutekeleza sera zetu. Sisi hatuna kinyongo kama wanatumia sera zetu kuongoza nchi hii, kwa sababu hatimaye anayenufaika ni mwananchi na hiyo ndiyo furaha yetu. Lengo letu ni Watanzania hawa kunufaika na nchi yao,” alisema.

Alibainisha kuwa mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu waliposema kuwa wakiichukua nchi wangetoa elimu bure walijua wangefanya nini lakini CCM kwa mawazo mgando walibeza kwa madai haiwezekani.

Aliongeza kuwa CHADEMA ilisema ikichukua nchi itaangalia na kurekebisha mfumo wa kodi na kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ikiwemo mfuko wa saruji uwe sh 5,000.

Alisema chama chake kilitoa kauli hizo kwa kuwa kinaamini bati, nondo na vinginevyo kadhalika, vingeshuka bei. Alisisitiza kuwa ni suala la formula na mfumo wa ulipaji kodi na uzalishaji viwandani, hilo nalo walibeza na wakasema haiwezekani lakini sasa wanatekeleza.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO