Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, mwanadada Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee ‘Anaconda’ ametangaza kuahirisha shughuli ya maadhimisho ya miaka 13 tangu aanze muziki iliyokuwa imapangwa kufanyika Ijumaa hii ya Mei 31, 2013 katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge kupisha msiba wa kifo cha msanii Albert Robert Mangweha aliyeripotiwa kufariki nchini Afrika Kusini jana.
Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
Jaydee ameeeleza uamuzi wake wa kutitisha show hiyo kuwa unalenga kutoa nafasi kwa wafiwa wote na wadau wa tansnia ya muziki na wapenzi wa Mangwea kumaliza taratibu za kumsitiri kipenzi chao na kueleza kwamba tarehe nyingine ya shughuli hiyo itatangazwa baadae.
Tangu amekaribishwa studio, Judith Wambura alionekana kuwa na majonsi sana kiasi cha kushindwa kuongea mara kwa mara na kukatisha mazungumzo yake kutokana na kukabwa na kilio.
Sherehe ya miaka 13 ya Lady Jay Dee katika muziki ilipangwa kuambatana na uzinduzi wa album yake ya sita inayo kwenda kwa jina la NOTHING BUT THE TRUTH ambayo ina jumla ya nyimbo 10, na pia kungekuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.
Bango la matangazo ya sherehe hiyo ya Lady Jaydee iliyoahirishwa ambapo mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV.
0 maoni:
Post a Comment