Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA ndicho chama tawala Tanzania mwaka 2015

 

Mimi ni Mtanzania kwa kuzaliwa, nimezaliwa, kukua, kusoma na kuishi Tanzania huku kwa umri wangu mdogo nikishuhudia mambo mengi yanatendeka katika Taifa letu lijulikanalo kama Taifa lenye amani Duniani kote.Huku tukihubiri amani, dhana yenyewe amani inaonekana kutofahamika kwa watanzania walio wengi; amani wakati watu wanakufa njaa; amani wakati raslimali za Taifa zinataifishwa na watu waliopewa dhamana ya kuzilinda na kuzipeleka nje kwa manufaa yao; amani wakati wananchi walio wengi wanashindwa kusomesha watoto wao shule nzuri; amani wakati vyombo vya ulinzi na usalama vinatumiwa na watawala wa kisiasa kuzima sauti za wananchi kwa kuwazuia kufanya mikutano , maandamano na hoja zenye maslahi kwa Taifa.

Yapo mambo mengi sana yanayoendelea kufanyika katika Taifa letu kupitia mgongo wa kuwadanganya watanzania eti ni nchi ya amani huku wachache wakitumia turufu hii ya tulinde na kudumisha amani ya Tanzania wakionekana wazi kabisa kuwa kujinufaisha na raslimali zetu tena bila huruma.

Nimezichambua sera za Chama tawala kwa hivi sasa Tanzania, utekelezaji wa sera hizo, muelekeo wa chama hicho, aina ya viongozi wanaoendelea kukiongoza na wanaoteuliwa kupewa nyadhifa mbalimbali nikagundua kuwa chama tawala Tanzania kilichopo kwa sasa mwisho wake huenda ni 2015 na kinawezakana kisiongoze hata kambi ya upinzani Bungeni.

Lakini pia nimechambua sera, utekelezaji na uwajibikaji, aina ya viongozi na namna viongozi wanavyowajibika kwa maslahi ya wananchi kwa kuvichunguza vyama vya upinzani vilivyoko hapa Tanzania na kugundua kuwa tayari vyama vingine vimebeba kofia ya upinzani lakini si vyama vya upinzani hata kidogo.Mfano, CUF ni chama ambacho kimeunda serikali ya mseto huko Tanzania visiwani lakini eti kikija huku Bara ni chama ya upinzani, katibu wake mkuu ndiye makamu wa Rais Zanzibar kwa maana hiyo huku Bara kikijadiri jambo kama chama cha upinzani basi habari na mikakati yote lazima awe nayo mh.makamu wa Rais huko Zanzibar.Kwa maana hiyo tayari kimepoteza taswira,lakini chama hiki kiliwahi kushika mashiko katika nchi hii kabla ya ccm kukishikilia bango kuwa ni chama cha waislamu na magaidi hivyo kukidhoofisha kabisa. NCCR-MAGEUZI nacho ni chama kilichoonekana kuwa na machachari kidogo chini yake Mh.James Mbatia kama mwenyekiti na kuwa na wabunge ambao kimsingi tunawaona wakijali maslahi ya Taifa lakini kitendo cha Mh.James Mbatia kuteuliwa mbunge la Rais wa ccm kilimuondolea baadhi ya element licha ya kwamba mh.Mbatia ni mtu anayeonekana kuwa na uzalendo wa Taifa hili mbali na itikadi za vyama na mambo mengine.Tunfahamu kazi nzuri anayofanya bwana Mbatia bungeni na hata nje ya Bunge ila tunashuhudia baadhi ya hoja zake zikikejeliwa na wabunge hata mawaziri wa ccm kwa kuwa na dhana ya kuwa kateuliwa na Rais ambaye ndiye mwenyekiti wa ccm.Mfano siku moja waziri alikuwa akijibu swali la mh.Mbatia bungeni na kusema,'mh.Spika, naomba kujibu swali la mh.James Mbatia, mbunge aliyeteuliwa na Rais wetu na mwenyekiti wetu wa ccm kama ifuatavyo'.Maelezo ya waziri huyu ilikuwa ni kumdisvalue bwana Mbati.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO(CHADEMA) ndicho chama pekee cha upinzani kilichobakia Tanzania kwa hivi sasa na ndicho chama kinachoonekana kukubalika zaidi kwa wananchi kila uchwao.Chama hiki kinazo sera, mikakati ya kuongoza nchi na viongozi wanaokubalika katika jamii wanaojulikana kama watetezi wa wanyonge na ndio maana mikutano ama maandamano yoyote yanayoitishwa na CHADEMA lazima wananchi waitikie kwa nguvu zao zote hata michango wananchi hukichangia chama hiki bila hiyana yoyote huku wakiwa na imani kabisa myoyoni mwao kuwa chama hiki chaweza kuwaletea matumani yao yaliyopotea.Ni kwa kufahamu hili cham cha mapinduzi chama hiki cha CHADEMA wanakiona sumu kwao, tishio kuliko maelezo, kinakubalika kuliko chenyewe chama tawala, kinaendelea kupewa misaada kutoka ndani na nje; ni kwa kufahamu hilo ndipo hujuma mbalimbali zilianza kutolewa kwa CHADEMA kwamba ni chama cha kikabila yaani wachaga(hoja iliishiwa nguvu), kuwa ni chama cha udini(hoja ilipuuzwa), ni chama cha marafiki(hoja iliishiwa mashiko), ni cham cha magaidi (HOJA ILIYOSHIKILIWA BANGO NA MAKADA WA CCM KAMA KETE YAO YA KUKIMALIZA CHADEMA, LAKINI WAMEANGUKIA PUA NA SASA VINYWA VYAO NVI WAZI WANADUWAA WAFANYE NINI MAANA CHAMA CHAO KINAWAFIA MIKONONI).

Ni kwa nini chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kinapewa kete ya kutawala nchi hii 2015? Hoja ni nyingi mno na sababu ziko wazi kabisa.Hii ni kutokana na Watanzania kuchoshwa na dhuluma za viongozi wa ccm na serikali kwa ujumla kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kuwaletea maendeleo na kuanza kujinufaisha wao wenyewe na vizazi vyao.BAADHI YA MAMBO AMBAYO YANAWADSIVALUE CCM NA KUWAVALUE CHADEMA NI KAMA IFUTATAVYO:

1.UCHAGUZI WA SPIKA WA BAADA YA CHAGUZI MKUU WA 2010.

Hakuna mtanzania ambaye hakuona dhuluma iliyofanyika ya kumuondoa mh.Sitta kugombea Uspika.Hizi zilikuwa ni mbinu chafu zilizofanywa na viongozi wa ccm wa juu na serikali kuhakikisha kuwa Bwana Sita hapati uspika maana alionekana kucheza kete zake vizuri bungeni kwa kuwapa haki sawa wabunge kujenga hoja huku wapinzani wakionekana kuichachafya serikali hadi kufikia kuiwajibisha pale waziri mkuu kwa wakti huo Mh.Lowasaa alipolazimika kujiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND. Hivyo walilazimika kuweka mtu ambaye atakahikisha kuwa analinda cham tawala kwa kuwaziba midomo wapinzani na hii ndiyo tunashuhudia maana Anna Makinda na Timu yake ya kina Ndugai inaonekana wazi namna inavyolinda serikali na ccm badala ya kufanya kazi ya kuwatumikia watanzani kuhakikisha wanaisimamia serikali.Wabunge wa ccm sasa hivi wanafanya kazi ya kuijibia hoja serikali na kuishauri, wajibu ambao ni wa mawaziri.Pale wapinzani wanapochachamaa juu ya serikali kutotimiza wajibu wake kwa wananchi tumeshuhudia wakipewa rungu kali na kiti cha spika, mambo haya huwapa credit CHADEMA huku nje ya Bunge kwa kutathmini kazi nzuri wanayofanya.

2.SERA YA CCM YA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

Baada ya serikali ya ccm kuingia madarakani kwa kete ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania, sasa imebainika kuwa ccm walikuwa wanomba kuingia madarakni ili kuleta maisha duni kwa kila mtanzania.Badala ya maisha bora kwa kila mtanzani kwa hivi sasa maisha yamekuwa magumu kuliko hata ya miaka iliyotangulia.Viongozi wa serikali na ccm wanashuhudiwa waziwazi wakijihusisha na vitendo vya ufisadi vya kuhujumu Taifa, wengine wanafanya biashara ya meno ya Tembo huko ulaya bila Taifa kunufaika na chochote(Mfano kwa mujibu wa hotuba ya kambi ya upinzani iliyowasilishwa na waziri kivuli mh.Mchungaji Msigwa ilimtuhumu Kinana ambaye ni katibu wa ccm Taifa kuhusika na ujangili wa nyara za Taifa letu huku serikali ikitoa majibu mepesi). Watanzania wanaona na wamechoka sana kuendelea kukitumika ccm na ndio maana wako tayari kukiweka CHADEMA madarakani 2015.

3.MATUMIZI MABAYA YA VYOMBO VYA DOLA.

Hili ni suala ambalo limekera si watanzania tu bali hata watu wa Mataifa ya nje.Tanzania inayomatumizi mabaya ya vyombo vya kwani tumeshihudia vyombo vya ulinzi na usalama vikifanya kazi ya kukilinda ccm kwa hali yoyote ile kwa kuwadhibiti wapinzani na wananchi kwa ujumla wasijumuike kujadili mambo ambayo yanahusu mustakabali wa Taifa letu.Vyombo hivyo vimefikia hatua ya kukiuka haki za binadamu kwa kuwaua baadhi ya watu wasio na hati Mf. maauji ya huko Arusha, Morogoro, MWANDISHI WA Habari MAREHEMU MWANGOSI ambaye aliuawa na jeshi la polisi kule Nyororo bila huruma huku tukio hilo likishuhudiwa na kamanda nduli na fashist KAMUHANDA wa mkoa wa Iringa huku serikali ya ccm ikijigamba kupitia kwa waziri wa mambo ya ndani Bwana NCHIMBI na waziri LUKUVI kuwa kamanda KAMUHANDA ni kiongozi shupavu anastahili pongezi kwa kuwadhibiti wapinzani kufanya mikutano.Watanzania walifadhaishwa na kifo cha Mwangosi na utekaji na utesaji wa mwenyekiti wa madaktari Dr.Ulimboka ambaye aliteswa sana lakini alipopata nafuu aliwataja wahusika wakiongozwa na maoisa wa IKULU ya Kikwete huku serikali ikibaki kimya juu ya Unyama huo.Watanzania wamekasirishwa na hali hiyo ya vyombo vya dola kuendelea kuwaziba midomo watu wanaoikosoa serikali ili kuhakikisha ccm kinaendelea kutawala hata kwa mabavu, wananchi wameamua 2015 CHADEMA ndicho chama kitachoongoza taifa hili ili kuliletea ukombozi dhidi ya watu wanaoendelea manyanyaso kwa raia wake tena bila huruma.

4.RAIA KUBAMBIKIZWA KESI NA VIONGOZI WA SERIKALI.

Serikali mahali popote pale ilipo duniani lengo lake ni kulinda utu, mali na haki za kila raia wake.Hali hii ni tofauti kabisa kwa Tanzania maana wimbi la viongozi wa serikali wakisaidiwa na vyombo vya dola la kuwabambikizia kesi za mauaji, ugaidi, ubakaji, rushwa tena kwa manufaa ya ccm limeshamiri.Waziri Nchimbi alilazimika kuwaondoa madarakani baadhi ya polisi waliokuwa wakiwabambikizia kesi wananchi kwa makosa ambayo hawajanfanya ili kujinufaisha lakini waziri hajua kwamba huo ni mtandao mrefu yani kuanzia chini mpaka juu serkali hivyo bado tatizo linaendelea.Mkurugenzi wa Ulinzi na usalam wa CHADEMA Mh.Lwakatare alibambikiziwa kesi ya UGAIDI na mafisadi wa ccm wakiongozwa na Mwigulu njemba ambaye anajifanya mzalendo kumbe ni fisadi mkubwa sana katika Taifa let kwa kuendesha siasa za kipumbavu ambazo hazina tija kwa Taifa letu.Ukweli umebainika Lwakate makosa ya Ugaidi kafutiwa na mahakama huku vyombo vya usalama ambavyo vilifanya kazi kubwa kuandaa ushahidi wa kupika wakihaibika.Vilevile baadhi ya polisi Morogoro wanashikiliwa wakiwa na kichwa cha binadamu ambacho walikuwa wanakwenda kumbambikizia mfanyabishara mmoja ili wamuombe rushwa kwamba wamemkata na kicha cha mtu mungu alisaidia wakatiwa mbaroni.Hali ni mbaya sana kama viongozi walinda amani ndio wanafanya uharamia huu wananchi wakimbilie wapi tofauti na kuiondoa serikali ambayo imeshindwa kuwajibika wa raia? CHADEMA NDO MBADALA 2015 kuondoa dhuluma hizi.

5.RUSHWA ILIYOKITHIRI, HUDUMA MBOVU ZA KIJAMIINA MIPANGO ISIYOTEKELEZEKA NA KUONGEZA UMASKINI.

Katika zama hizi za serikali inayoongozwa na ccm suala la Rushwa limeishaonekana kuwa ni huduma maana hata wabunge wa ccm walishataka kupisha sheria eti ni takrima.Huwezi kupata huduma popote pale mpaka utobolewe mifuko yako,Vituo vya polisi, mahakamani, mahospitalini ,mashuleni, maofisini rukshwa imeshamiri na hakuna juhudi za makusudu kukomesha tatizo maana hata TAKUKURU ni wala rushwa wakubwa sana.

Elimu yetu imeishaonekana si chochote wa lolote.Wanafunzi wamefanya mitihani kidato cha nne zaidi ya nusu walipata 0 baadaye serikali ya ccm kifuta matokeo na kuanza kuchakachuaa matokeo mapya hivi sasa tunasubiri uchakachuzi huo ukamilike tuone jipya ni lipi, swali ni je hata mwaka kesho watachakachua?

Kimsingi mambo ni mengi LAKINI KIKUBWA NI KWAMBA WANANCHI WAMEISHAJIPANGA 2015 LKUKIWEKA MADARAKANI CHADEMA ILI KUNUSURU TAIFA HILI NA HAWA WAFEDHURI WACHAHCHE.


Imeandikwa na Jose Kasano

Chanzo: Kong’oli Hapa

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO