Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wakati Mh Mbowe Akiendelea na Ziara Jimboni Kwake, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willbroad Slaa nae Kuanza Ziara Mkoa wa Manyara Kesho

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willbroad Slaa ziarani Mkoa wa Manyara


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbroad Slaa, anatarajiwa kuanza ziara ya ujenzi na kukagua uhai wa chama katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Mkoa wa Manyara, siku ya Jumamosi, tarehe 18-26, Mei 2013

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Dkt. Slaa ataambatana na watendaji wa Makao Makuu ya CHADEMA pamoja na wabunge wote wa CHADEMA Mkoa wa Manyara.

Akiwa katika ziara hiyo, mbali ya kupokea taarifa na kukagua uhai na ujenzi wa chama katika maeneo atakayopita, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara takriban miwili kwa kila siku pamoja na mikutano ya kikazi ya ndani, ambapo atakutana na wanachama na viongozi wa maeneo husika.

Ratiba ya ziara hiyo itakuwa kama ifuatavyo;

Atawasili Babati Mjini 18/5/2013 asubuhi; ambapo kutakuwa na mapokezi na kisha salamu kwa wananchi eneo la Minjingu, baadae atakuwa na mkutano wa hadhara saa 9 mchana viwanja vya Kwaraa, Babati mjini.

Akiwa njiani kuelekea Hanang, tarehe 19/5/2013, Katibu Mkuu atapita na kuwasalimia wananchi wa maeneo ya vijiji vya Masqaloda, Measkron, Nangwa na Dirma, kabla ya kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Balangida na Gendabi (Hanang).

Tarehe 20/5/2013, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atafanya mikutano ya hadhara Basutu (Hanang) na Haydom (Mbulu).

Siku ya tarehe 21/5/2013, Katibu Mkuu wa CHADEMA atakuwa na mkutano wa hadhara Dongobesh na Mbulu Mjini.

Tarehe 22/5/2013 akiwa njiani kuelekea Babati Vijijini, Katibu Mkuu atawasalimia wananchi wa vijiji vya Mutuka na Mwikansi kabla ya kufanya mkutano wa hadhara Galapo, Babati Vijijini, kuanzia saa 8 mchana.

Siku ya tarehe 23/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara maeneo ya Riroda, Dareda na Bashnet, Babati Vijijini.

Tarehe 24/5/2013, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Simanjiro na atafanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Musitu wa Tembo, Ngorika na Ngage.

Siku inayofuata, tarehe 25/5/2013, Katibu Mkuu atakuwa na mikutano ya hadhara katika maeneo ya Orkesimet, Namaruru kisha atamalizia kwa kufanya mkutano mkubwa Mererani, kuanzia saa 10 jioni.


Imetolewa leo, Mei 17,2013 na;


Tumaini Makene

Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA


Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO