Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kampeni za Udiwani Kanda ya Kaskazini: Lema aongoza kikosi cha Chadema Kata ya Makuyuni kubomoa ngome ya Lowassa akitumia ‘Chopa’

kamapeni Makuyuni (6)Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mh Godbless Lema akimnadi mgombea wa chama chake katika uchaguzi wa marudio Udiwani Kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli, Mwl Sironga (mwenye kombati) katika mkutano mkubwa uliofanyika Makuyuni Jumamosi ya Mei 25, 2013. Mh Lema aliwasili viwanjani hapo na usafiri wa Helcopta majira ya saa 9:30 alasiri. Katika mkutano huo Lema alisema Chadema imejiandaa kushinda katika Kata hiyo na hawataruhusu kura hata moja kuibiwa, kwasababu itakuwa ni kutowatendea haki wazee wa kimila waliobariki na kuiunga mkono Chadema badala ya CCM kama ilivyozoeleka.

kamapeni Makuyuni (1)Mh Lema akitoka kwa tahadhari ya kiusalama kwenye “chopa” iliyomfikisha Makuyuni tokea Moshi alikohudhuria msiba wa mjomba wake

kamapeni Makuyuni (2)Wazee viongozi wa kijamii (ma-Leigwanani), viongozi wa Chadema Makuyuni na wageni kutoka Arusha Mjini, akiwemo Mbunge Lema wakiwa meza kuu katika mkutano huo.

kamapeni Makuyuni (3)Kutoka kushoto, Mratibu wa shughuli za wanawake Chadema Mkoa wa Arusha, Mh Cecilia Ndossi, Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema, Katibu wa Kanda ya Kaskazini, Mh Amani Golugwa na wa mwisho ni mgombea wa Chadema Kata ya Makuyuni, Mwl Sironga

kamapeni Makuyuni (4)Baadhi ya wananchi wa Makuyuni wakifuatilia hotuba za viongozi waliokuwa wakihutubia mkutanoni

kamapeni Makuyuni (5)Mh Lema akiwajibika jukwani kumnadi mgombea wa Chama chake Kata ya Makuyuni, Mwl Sironga. Kwa mujibu wa maelezo ya wananchi wengi waliohojiwa na Blog hii mkutanoni hapo, wanaonekana kuendelea kumuunga mkono mgombea huyo ambae awali alishinda kura za maoni CCM alkini jina lake likaondolewa na kupewa mshindi wa tatu na hivyo kumasha hasira kwa wananchi hao.

kamapeni Makuyuni (7)Mgombea wa Chadema kuwania Udiwani Kata ya Makuyuni-Monduli, Mwl Sironga Leimburuki akihutubia wananchi waliojitokea kwenye kutano wa hadhara uzinduzi rasmi wa kampeni za Chadema katika Kata hiyo Jumamosi ya Mei 25, 2013. Awali Mwl Sironga alikuwa mgombea wa nafasi ya kuiwakilisha CCM aliyeongoza katika kura za maoni lakini baadae jina lake likaondolewa na nafasi yake akapewa aliyekuwa mshindi wa tatu.

Mgombea huyu, Mwalimu mwenye degree moja na mzawa wa Makuyuni, aliahidi kufuatilia ardhi yote inayotaka kuporwa ama iliyoporwa na kusaidia vijana waliokosa ardhi kuipata kwa shughuli za ufugaji na maendeleo.

kamapeni Makuyuni (8)Mbunge wa Arusha Mjini ambae alikuwa mgeni mkuu katika kampeni hizo, Mh Godbless Lema akisikiliza kwa makini mawaidha ya Leigwanani Sewinge kutoka Liwini-Makuyuni aliyekuwa akitoa baraka za kimila kwa mgombea wa Chadema na chama chake siku ya Jumamosi Mei 25, 2013. Jumla ya viongozi wazee wa kijamii (leigwanani) watatu walipata nafasi ya kutoa baraka zao

 

kamapeni Makuyuni (9)Huyu ni kiongozi mwigine wa Kimila, Leigwanani Samwel Keeje kutoka Naiti-Makuyuni akitoa baraka zake pia kwa mgombea wa Chadema, Mwl Sironga na chama chake katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni katika Kata ya Makuyuni siku ya Jumamosi Mei 25, 2013. Leigwanani Keeja hakuweza kutumia kiswahili na hivyo ikalazimu kuwe na mkalimani. Katika moja ya nukuu zake, alisema “Pokea hii rungu ya Chadema kuwa nguzo kuu muishinde CCM” na kisha kumkabidhisha Mwl Sironga kwa watu waliohudhuria mkutano huo jamii yake.

Picha zote na SeriaJr, Makuyuni-Monduli


MAGAZETINI: MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbles Lema, amewataka wakazi wa kata ya Makuyuni kumchagua Japheti Sironga kuwa diwani wao ili kuleta ukombozi wa wananchi jamii ya kimasai.

Lem alitoa kauli hiyo juzi katika uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi huo mdogo.

“Safari hii hata sisi tulipata mshtuko kwa kupata mgombea msomi mwenye master (shahada ya Uzamili) ambaye ameamua kwa dhati kurejea nyumbani kuomba ridhaa ya kuwakomboa ndugu zake. Sasa ni wajibu wenu wananchi kumchagua, ili dhamira yake kwenu itimie,'' alisema Lema.

Aliwahakikishia wananchi wa Makuyuni siku moja baada ya kumchagua Sironga kuwa diwani atakwenda naye mjini Dodoma kumkutanisha na mawaziri, ili awasilishe kero zao ambazo zimekua sugu.

Naye mgombea huyo, Japheti Sironga, akiwahutubia wananchi na kuomba kura aliwaahidi kuwa kazi yake kubwa ya kwanza wakimchagua ni kuhakikisha rasilimali ardhi iliyopo Makuyuni inawanufaisha wananchi wote.

“Mkinichagua nitakikisha ardhi yote ambayo hivi sasa inamilikiwa kinyemela na vigogo wa Monduli ikiwemo Ranchi ya Manyara inakuwa ya manufaa kwa wananchi wote,”alisema.

Kuhusu kero ya maji, alisema atahakikisha anafuatilia miradi yote ambayo ilikabidhiwa kwa wawekezaji ambao hawafahamiki walipo ili kujua fedha za miradi hiyo zimeliwa na nani na kuwafikisha katika vyombo
husika.

Alisema Rais Jakaya Kikwete alipokwenda Makuyuni alipewa shukurani na mbunge wa Monduli, Edward Lowasa kuhusiana na mradi wa sh bilioni mbili uliopelekwa katika kata hiyo, lakini mpaka sasa mradi huo haujulikani ulipo, hivyo itakua jukumu lake kufuatilia mradi huo kuona unafanya kazi.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO