Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: ASKARI POLISI MSTAAFU ALIVYOCHARANGA MAPANGA MWANAE WA MIAKA 4 KWA SABABU YA WIVU WA KIMAPENZI (TUNAOMBA RADHI KWA BAADHI YA PICHA)

KAHAMA

Mkazi wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi.Endelea kupitia audifacejackson blog.Tukio hilo limetokea leo jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness (28) Elias huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.Endelea kupitia audifacejackson blog.Kwa mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.

Imefafanuliwa kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani.Endelea kupitia audifacejackson blog.Majirani kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.

Hata hivyo Wakati gari la Poisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.

Mtoto Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.na mwanaafrika

MTOTO WA MIAKA 4 DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI KWA HUDUMA AYA KWANZA.

 

WANANCHI WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA WILAYA WAKIWA NA SHAUKU YA KUMUONA MTUHUMIWA.

KINA MAMA WALIOGUSWA NA TUKIO WAKIWA NJE YA HOSPITALI KUMUONA MTOTO HUYO.

AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI

HAPA AFANDE AKIWA HOI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI..

MADAKTARI WAKIJITAHIDI KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.

MADAKTARI WAKIWA KAZINI KUHAKIKISHA WANAOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.


AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI HUKU AKIWA AMEFUNGWA PINGU.

JITIHADA ZA KUOKOA MAISHA YA MTOTO ZIKIENDELEA

INASIKITISHA SANA JAMANI

MAJUKUMU YA KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO YAKISONGA KWA KASI.

AFANDE BWIRE AKIWA NA PINGU ZAKE WODINI


MUNGU AMPE AHUENI MTOTO HUYU.

PICHA ZOTE NA MAELEZO: JACKSON AUDIFACE BLOG

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO