Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA CLOUDS MADE IN TANZANIA KUPINGA UHARAMIA WA KAZI ZA SANAA MJINI DODOMA.

Baadhi Wadau wa Muziki na Filamu wakiwa na mabango yao yaliyobeba jumbe mbalimbali mapema leo kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea


Baadhi ya Wasanii wa Filamu hapa nchini Wema Sepetu sambamba na shosti yake Kajala walikuwa ni miongoni mwa wasaani waliounga mkono matembezi hayo ya mshikamano yaliyokuwa yametawaliwa pia na mabango kadhaa yaliyobeba jumbe mbalimbali za kupinga wizi wa kazi sanaa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akiwakaribisha watu wote waliofika kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Waziri Mkuu Pinda.

Baadhi ya magari yakiwa yamesimama yakipisha matembezi ya mshikamano yaliyokuwa yakielekea kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana.


Baadhi ya Watangazaji wa clouds FM,sambamba na wasanii wa muziki wa kizazi kipya/tasnia ya filamu na wadau wengine wa sanaa wakiwa wamejumuika kwa pamoja kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Mh Waziri Mkuu Pinda.

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni na Mdau mkubwa wa sanaa hapa nchini,Mh.Idd Azan akiunga mkono harakati za kupapambana na maharamia wa kazi za sanaa hapa nchini

Gari ya Waziri Mkuu Pinda ikiwasili

Waziri Mkuu Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari,Vijana, michezo na Utamaduni,Mh.Amos Makala habari,Michezo mara alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana mjini Dodoma. 

Waziri Mkuu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Vipindi na utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba mara alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana mjini Dodoma.

Mmoja wa Watangazaji wa kipindi cha Jahazi,Wasi Wasi Mwambulambo akiserebuka na Mh.Rehema Nchimbi.

Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi,kulia mtangazaji wa Clouds FM Mbwiga Mbwiguke na Shaffih Dauda (shoto) wakitwibiwirika kwa pamoja mapema leo mchana mjini Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere skwea.

Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM (wote waliosimama nyuma).Reedio Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa TWENZETU  kwa minajili ya kuielimisha jamii  kuwa na tabia ya kupenda vya kwao na  kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA kujikwamua kimaisha.

CREDIT: BOSS NGASSA WA DODOMA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO