Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MBUNGE MSIGWA AMTAKA KINANA KWENDA MAHAKAMANI KESHO


Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amemtaka  katibu mkuu  wa chama  cha mapinduzi (CCM) Bw  Kinana  kutosubiri muda  wa  siku  21 alizozitoa  kumfikisha mahakamani kuwa  yupo tayari  kwenda mahakamani hata kesho.

Mbunge Msigwa amesema kuwa katika  ukweli kama  hata  kuwa tayari kumwogopa mtu na kuwa siku  zote atasimama katika  ukweli katika  kupigania maslahi ya Taifa  hili.

Mbunge  Msigwa amesema  kuwa hatua ya katibu mkuu  wa CCM kukimbilia katika  vyombo  vya habari  kutishia  kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika  kupelekewa taarifa  ni  sawa na kumwogopa na  hivyo suala la Kinana kwenda Mahakamani  si  sawa ni  kumtishia nyau mtu mzima.

Kwani  alisema  kuwa  Chadema  ina  mawakili  waliojitosheleza na  kuwa hawatanyamaza kusema  ukweli kwa  kuogopa vitisho vyovyote .

Aidha mbunge huyo amewataka wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga ) mjini Iringa kuendelea kufanya kazi katika eneo la Mashine tatu bila kufanya vurugu zozote kwa wale wanaozuia kufanya hivyo.
Akizungumzia suala la Machinga kuendelea kunyanyasika mbunge Msigwa amesema kuwa tayari suala hilo ameanza kulipigania bungeni kwa waziri mwenye dhamana hivyo kamwe machinga Iringa wasikubali kunyanyasika .

Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi  wa  jimbo hilo jioni hii katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya mikoani

Umati mkubwa  wa  wananchi  wakimsikiliza mbunge  wao wa  jimbo la Iringa mjini

Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini Mchungaji ,Msigwa akiwahutubia  wananchi  wa  jimbo la Iringa mjini

CHANZO: FRANCIS GODWIN

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO