Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Rais Kikwete ahudhuria kikao cha SADC jijini CAPE TOWN

Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(Watatu kushoto) akiongoza kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC kilichofanyika jijini Cape Town Afrika ya Kusini leo.Wengine katika picha ni wajumbe wa kamati hiyo akiwemo mwenyeji Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini(kulia),Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Namibia Bibi Netumbo Nandi-Ndaitwa(kushoto) na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dkt.Tomaz Salomao.

Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC Dkt.Tomaz Salomao mjini Cape Town Afrika ya Kusini leo wakati wa kikao cha kamati hiyo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini wakitoka katika ukumbi wa hoteli ya Westin jijini Cape Town Afrika ya Kusini mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalma ya SADc kilichofanyika leo.Rais Kikwete alikuwa nchini Afrika ya Kusini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mkurugenzi Mtendaji na mratibu wa asasi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bwana Mark Suzman jijini Cape Town Afrika ya Kusini.Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Adam Malima.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagana na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Misaada la Marekani USAID Dkt. Rajiv Shah muda mfupi baada ya kufanya naye mazungumzo katika ukumbi wa Cape Town Convention Centre jana.Picha na Freddy Maro.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO