Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Ni kosa kuomba kura kwa udini, ukabila-Lema

DSC07088Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema, amewaonya wagombea udiwani wa chama hicho, katika kata nne jijini la Arusha, kuacha kutoa ahadi zisizotekelezeka katika kampeni zao. Pichani Mh Lema akihutubia wananchi wa Kata ya Kaloleni eneo la nyuma ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Picha na SeriaJr


Gazeti Mwananchi linaripoti Mei 30, 2013

Kata ya Elerai

Akizungumza katika kampeni zilizofanyika Kata ya Elerai jana, Lema ambaye anaongoza kampeni za Chadema kwa sasa katika kanda ya Kaskazini, kabla ya timu ya viongozi wengine wa kitaifa kufika, alisema ni heri kutokupata kura kuliko kuwadanganya wananchi kwa kutoa ahadi za uongo.

Lema pia aliwaonya wagombea hao, kuacha kuomba kura kwa misingi ya udini, ukabila ama ukanda kwani, hakuna mgombea ambaye anaweza kushinda kwa kuungwa mkono na dini moja au kabila moja pekee.

“Hakuna kosa kubwa kwa sasa katika siasa kama kuomba kura kwa udini au ukabila, mkifanya hivyo mtapotea na sisi hatutawaunga mkono,” alisema Lema.

“Ukweli unadumu daima, kama kuna watu wanasema hawakuchagui hadi uruhusu biashara ya mirungi au uwape mkopo wa kupika gongo, bora wasikuchaguwe kabisa,” alisema Lema.

Alisema wagombea hao, kama wakitoa ahadi za uongo, watasababisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 uwe mgumu kwa chama hicho kwani hawataweza kutimiza ahadi.

“Hatutaki uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 uwe mgumu kwetu, mimi mwaka 2005 nilishindwa kwa kukataa kutoa ahadi za uongozi, lakini mwaka 2010 nimechaguliwa kuwa mbunge yale walioahidi wenzangu walishindwa kutekeleza,” alisema Lema.

Katika kampeni hiyo, mgombea wa udiwani wa Chadema katika kata ya Elerai, Jeremiah Mpinga, aliomba wakazi wa kata hiyo, kumchagua kwani anajua matatizo yao.

Hata hivyo, Mpinga anakabiliwa na upinzani mkali katika kata hiyo, toka kwa mgombea wa udiwani wa CUF, John Bayo ambaye alikuwa ni mmoja wa madiwani watano wa Chadema waliofukuzwa uanachama.

Bayo ambaye amekuwa akiungwa mkono na makundi ya watu wa kati hasa kutokana na misimamo yake, alisema jana kuwa ana uhakika wa ushindi na kurejea katika halmashauri ya Jiji.

“Nia yangu kubwa ni kurejea katika halmashauri kwa tiketi ya CUF ‘‘ alisema.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO