Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Soma hapa Ya Kinana kumkacha DK Slaa na Kisa cha Nape ITV

Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akisalimiana na kufurahia jambo na Katibu Mwenezi wa CCM Nape Moses Nnauye walipokutana katika Studio za ITV.Picha na Chadema

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amemkacha Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

Wawili hao walitarajiwa kukutana kwenye kipindi kipya kiitwacho ‘Uzalendo’, kinachotarajiwa kuanza kurushwa wakati wowote kuanzia mwezi ujao katika kituo cha televisheni cha ITV.

Taarifa za Kinana kumkimbia Dk. Slaa katika mdahalo huo zilisambazwa jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini.

Taarifa hiyo na vyanzo vyetu vingine vya habari, vilieleza kuwa viongozi hao walialikwa na ITV kwa ajili ya mdahalo ambao ungerekodiwa na baadaye kurushwa na kituo hicho.

Kwa mujibu wa habari hizo, viongozi hao walipewa mwaliko wa kuhudhuria kipindi hicho siku kumi zilizopita na wote kuthibitisha ushiriki wao, lakini Dk. Slaa jana alifika katika studio za kituo hicho na kukutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, badala ya Kinana.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana, Dk. Slaa alisema: “Ni kweli tulikuwa tumealikwa kwenye mdahalo pale ITV (leo) jana saa 3, nilipofika nilikutana na Nape, nikamsalimu nikajua kuwa alikuwa amemsindikiza Kinana, lakini nilipomuuliza mwendesha kipindi kwamba Kinana yuko wapi, alisema amepata udhuru hivyo hajafika.

“Nilimwambia Nape wewe si saizi yangu, sitaweza kuongea katika kipindi hiki kama Kinana hayupo, hivyo kipindi hiki kiahirishwe hadi Kinana atakapokuwa na nafasi ya kuja,” alisema Dk. Slaa.

“Haiwezekani mwenzangu akaahirisha ghafla kuja kwenye kipindui halafu nisipewe taarifa na badala yake nikatumiwa Nape, Nape si saizi yangu,” alisisitiza Dk. Slaa.

Taarifa zaidi zinasema kuwa baada ya kuahirishwa kipindi hicho, Nape na Dk. Slaa walisalimiana na kuagana. “Naamini siasa si uadui, niliongea na Nape nikamuuliza Kinana yuko wapi, alisema alikuwa amepata udhuru, akanipigia simu nije,” alisema.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo, Nape alisema alikwenda ITV badala ya Kinana, kuangalia maudhui ya kipindi hicho ili aweze kushauriana na Kinana na kuamua kuja au la.

“Mimi ndiyo msemaji wa chama, katibu mkuu hawezi kualikwa mimi nisiwe na taarifa, mimi ndiyo napaswa kwenda na nilikwenda nilipokutana na Dk. Slaa tukaelezwa, Dk. Slaa alishauri kuwa inafaa kualika watu wenye hadhi zinazofanana, yaani makatibu, hivyo mimi niliondoka nikamwacha Dk. Slaa, nadhani alirekodiwa kwa kuwa walisema wanaweza kurekodi mtu mmoja mmoja na katibu mkuu wetu anaweza kwenda siku nyingine kurekodi,” alisema Nape.

Kinana mwenyewe alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo, hakuweza kupatikana kwani simu yake iliita bila kupokewa.

Chanzo: Tanzania Daima Mei 16, 2013

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO