Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kesi ya Lema akidaiwa kuchochea vurugu Chuo cha Uhasibu Arusha yasoahirishwa hadi Julai 2, 2013

Hakimu Devota Msofe wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ameahirisha shauri la kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), kwa tuhuma za uchochezi hadi Julai 2, 2013 kesi hiyo itakapotajwa tena na shauri hilo kuanza kusikilizwa upelelezi ukiwa umekamilika.

Mwishoni mwa mwezi Aprili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa Arusha baada ya kukaa rumande tangu alipokamatwa usiku wa kumkia siku ya Jumamosi, Aprili 27, 2013 na kusomewa mashitaka ya uchochezi na kisha kuachiwa kwa dhamana siku hiyo ya Jumatatu ya April 29, 2013.

Katika kesi hiyo ya uchochezi, Lema anadaiwa kuwa Aprili 24, mwaka huu,  akiwa eneo la Freedom Square la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), alifanya kosa la uchochezi wa kutenda kosa kinyume cha kifungu namba 35 na 390 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kuwaeleza wanafunzi wa chuo hicho kuwa: “Mkuu wa Mkoa amekuja kama anakwenda kwenye send-off, hajui Chuo cha Uhasibu mahali kilipo wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo hiki. Ameshindwa kuwapa pole kwa kufiwa na kusikiliza shida zenu na amesema hawezi kuongea na wanafunzi wasio na nidhamu.”

DSC07067Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu (CHADEMA) akitoka Mahakamani na mawakili wake Humphrey Mtui na Method Kimomogoro asubuhi hii mara baada ya kesi inayomkabili kuahirishwa hadi Julai 7, 2013 ambapo upelezi utakuwa umekamilika na shauri husika kuanza kusikilizwa.

DSC07071Mh Lema akiongea na wakili wake, Wakili Method Kimomogoro nje ya viwanja vya Mahakama

DSC07069Wakili Method Kimomogoro anayemtetea Lema akisalimiana na mgombea Udiwani wa Chadema Kata ya Kimandolu, Rayson Ngowi baada ya kutambulishwa na Lema

DSC07075
Mgombea udiwani wa Chadema Kata ya Kimandoli Mch Rayson Elishadai Ngowi aliyemsindikiza Mh Lema Mahakamani hapo akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na mchakato wake wa udiwani. Mch Ngowi amesema kwamba ameadhimia kugombania udiwani ili kuweza kupambana na matataizo yaliyopo katika Kata yake akitaja vipaumbele vikuu  kuwa ni ubovu wa barabara, huduma za afya (hopsitali na zahanati) pamoja na kufukuzwa kwa wanafunzi (wasiojiweza) mashuleni kwa matatizo ya ada ambazo zipo Halmashauri.

Picha zote na SeriaJr, 29 Mei, 2013

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO