Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Rest In Peace Albert Mangwea… You Have Gone Too Soon Brother!

Taarifa za kifo cha msanii Albert Mangwea aka Mimi aka Cow Bama aka Cow Wizzy kilichotokea nchini Afrika Kusini jana zimepokelewa kwa huzuni kubwa na watanzania nchini kote, jiji la Dar es salaam limeshtushwa na taarifa hizo zinazotangazwa kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii. (Picha na Annapita.Com)

Albert Mangwea alifariki dunia jana hii katika hospitali ya St Hellen iliyoko South Africa, sababu za kifo chake hazijawa wazi mpaka sasa, ingawa redio nyingi jioni hii zinaeleza kuwa afariki akiwa usingizini na kwamba inahisiwa chanzo cha kifo chake ni kuzidisha dozi  ya dawa za kusisimua mwili.

Historia fupi

Jina lake halisi ni Albert Keneth Mangweha, ana asili ya Ruvuma (Mngoni) lakini alizaliwa Mbeya 16 Novemba 1982 akiwa mtoto wa mwisho. Kwa baba yake alikuwa mtoto wa 10 na kwa mama ni mtoto wa 6 kuzaliwa.

Akiwa na miaka 5 alihama Mbeya na kuhamia Morogoro na kusoma Shule ya Msingi Bungo hadi darasa la 5 na kisha kuhamia Dodoma akiwa na Baba yake na kumalizia Shule ya Msingi Mlimwa.

Alisoma Shule ya Sekondari na Chuo cha Ufundi Mazengo Mjini Dodoma.

Taarifa za msiba

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya taarifa, inaelezwa kuwa Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangwea ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani Baba Mkubwa wa Ngwair, David Mangwea ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika Dar es salaam Mbezi Beach.

Taarifa zinaeleza zaidi kuwa ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini Baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa. Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na Kaka yake yaani Baba Mkubwa wa marehemu.

Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika ya Kusini Baba mdogo amesema kuwa  tayari ndugu wameshaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania Afrika ya Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa nyumbani.

BLOG HII INATOA POLE KWA WAFIWA WOTE NA KUMUOMBA MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO