Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CHADEMA KWA UDIWANI WA KATA NNE ZA ARUSHA; CHADEMA WATUMIA CHOPA NA KUSISITIZA AMANI NA HAKI VITAWALE

chopa ikitua ngarenaro‘Chopa’ iliyotumiwa na Lema ikitua viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro muda mfupi kabla ya kuanza mkutano. Chopa hiyo ilizunguka anga la Jiji la Arusha kwa madoido ya aina yake, hususani katika Kata nne za Themi, Kimandolu, Elerai na Kaloleni, halikadhalika eneo la mkutano, huku ikimwaga vipeperushi vya kunadi kampeni za Chadema na wagombea wake. Blog hii ilishuhudia wananchi wakigombea vipeperushi hivyo vikitua chini.

umatiSehemu ya umati wa wananchi wa Jijini Arusha waliojitokeza jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro kuhudhuria Mkutano Mkubwa wa Chadema wa Uzinduzi wa Kampeni za kuwania Udiwani kwa Kata nne zilizoachwa wazi na madiwani waliovuliwa uanchama  na Chadema zaidi ya miaka miwili iliyopita.

DSC06845

DSC06855Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa kamati Kuu Chadema, Mh Godbless Lema akihutubia umati wa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo. Lema aliongelea mambo mengi kuhsiana na uchaguzi huo na siasa za nchi kwa ujumla huku akirudia kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa kinara wa udini nchini ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ambapo alitolea mifano ya kuwatapeli waislamu mwaka 2005 kwa ahadi hewa ya Mahakama ya Kadhi, na kampeni za mwaka 2010 alipodai kuwa kuwa kuna timu ya kampeni za mgombea wa CCM wakati huo zilipita kwenye mimbari za ibada na kuwahimiza waislamu wasimchague padri (akimaanisha Dr Slaa).

Akizungumzia chaguzi hizo, Mh Lema aliwatahadharisha viongozi wa Mkoa, Wilaya na Jeshi la Polisi kutojaribu kuingilia chaguzi hizo. Akadai kuwa akionewa mmoja watakuwa wameonewa watu wote na hivyo hawatakubali.

Aidha, Lema alizungumzia ‘msuguano’ wa udini nchini, na kusema kuwa suluhisho haliwezi kupatikana kwa kufanya propaganda. Alidai kuwa suluhu itapatikana kwa pande zote zinazohusika, akitaja Serikali na viongozi wa dini zote kukaa pamoja na kuelezana ukweli ili kupata suluhu ya kudumu. Lema alidai kamwe hataacha kusema ukweli kwa kuogpa kukosa kura kama wengine kwa kuwa kiongozi wa kweli hasemi uongo ili apate kura.

Mh Lema amezungumzia pia tuhuma dhidi yake na chama chake kuwa wanapenda fujo na maandamano, na kukanusha huku akifafanuo kuwa sio kweli kwamba wanapenda fujo na maandamano, bali hawapendi na hawakubali kuonewa au kudhulumiwa haki zao.

Mbunge huyo alifichua pia tuhuma za ufisadi mkubwa aliodai kuugundua kufanywa na Halmashauri ya Jiji la Arusha.

DSC06831Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, ambae pia ni Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Arusha na Diwani wa Kata ya Levolosi, Mh Ephata Nanyaro akihutubia mkutanoni hapo.

Nanyaro amewaeleza maelfu ya wananchi waliojitokeza viwanjani hapo kuwa wao kama Chadema hawaendi kushiriki uchaguzi, bali kushinda na kurudisha Kata zao ambazo ziliachwa  wazi baada ya chama chake kuwafukuza madiwani waliowakilisha Kata hizo kwa alichodai ni kupokea rushwa ili wahujumu Chadema katika sakata la kutafuata muafaka wa uchaguzi wa Meya waliodai kuwa batili na baadae kupelekea vifo vya watu watatu na makumi wakiwaki na mejeraha na wengine ulemavu.

Akisisitiza zaidi, Bw Nanyaro amedai kuwa lengo la Chadema ni kuzirudisha Kata hizo ili wapate nguvu ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya Gaudence Lyimo ili uitishwe uchaguzi upya. Alidai kuwa kwasababu Tume ya Uchaguzi imeonekana kumtambua aliyekuwa diwani wa kata ya Sombetini (Alphonce Mawazo aliyehamia Chadema toka CCM), basi wao Chadema watamuita Mawazo ahudhurie vikao vya Halmashauri kama awali, akiwa mwakilishi wa CCM lakini akifanya kazi ya Chadema.

Nae Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini Bw Martin Sarungi alipopewa nafasi ya kuongea alitumia nafsi hiyo kutahadharisha kwamba Chadema kupitia intelijensia yao wamegundua mbinu ovu za makusudi kuvuruga mikutano ya Chadema katika Kata tofauti kwa kuansiha vurugu ama kurusha mawe.

Sarungi aliwataka wapenzi wote wa Chadema kuwa walinzi wa amani katika mikutano yao yote ya Chadema na kwamba yeyote watakayemtilia shaka nataka kuvuruga amani watoe taarifa ama kumfikisha kwenye vyombo husika.

meza kuu

meza kuu1Meza kuu ya viongozi wa Chadema katika mkutano huo jana. Viongozi waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema, Madiwani wote wa Chadema, Viongozi wa chama ngazi ya Wilaya na Mkoa na wagombea wa chama hicho kwa Kata za Themi, Elerai, Kimandolu na Kaloleni.

lema na chopaMbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, mh godbless lema akiteremka kwenye helkopta iliyomleta viwanja vya Ngarenano ulikofanyika mkutano. Mtu mwingine aliyewasili na elkopta hiyo sambamba na Lema ni mgombea wa chama hicho Kata ya Elerai, Eng. Jeremia Mpinga.

DoitaKiongozi wa Madiwani wa Chadema Halmashauri ya Jiji la Arusha, Mh Doita akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kutowapa nafasi wanasiasa watakaowapelekea siasa za udini na ukabila.

DSC06820Mjumbe wa Kamati tendaji Wilaya na Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Sombetini, Bw Abdi Madava, Kata ambayo Tume ya Uchaguzi haijaitangaza kuwa miongoni mwa Kata zinazopaswa kurudiwa uchaguzi wake kwa madai kuwa hawakupata barua rasmi ya kuhama kwa  Diwani aliyekuwapo awali (Alphone Mawazo) kwa tiketi ya CCM na kuhamia Chadema zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

DSC06821Mwenyekiti wa Vijana (BAVICHA) Wilaya ya Arusha Mjini, Bw Noel Olevaroya akihutubia. Noel alisisitiza kuwapo kwa uchaguzi huru na wa haki. Alienda mbali zaidi na kudai kwamba kama vijana hawataki uchokozi wa aina yeyote na kwamba watakuwa watulivu lakini hawatakubali kuchokozwa.

DSC06822Mjumbe mwakilishi kutoka Arumeru Magharibi, ambaye ni Katibu wa Chadema Arusha Vijijini. Ujumbe wake ulihusu ushirikiano wa wa Arumeru Magharibi kuhakikisha wanasaidiana kupambana na hila zozote katika chaguzi hizo

DSC06824Mwakilishi toka Moshi ambaye alikuwa Meneja kampeni wa Mzee ndesamburo, maarufu kama Makelele alipata wasaa wa kuzungumza na wananchi wa Arusha mkutanoni hapo na kuwataka kutopoteza fursa hii muhimu kwao kuchagua viongozi ambao wataweza kuwawakilisha vyema na kutolea mfano wa mafanikio ya Halamashauri ya mji wa Moshi ambayo inaongozwa na Chadema kwa mafanikio makubwa.

DSC06859Mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bw Malance Kinabo

DSC06857Eng. Jeremiah Mpinga, Mgombea wa Chadema Kata ya Elerai akipanda jukwaani

DSC06871Mh Lema akitambulisha wagombea wa Chadema kwa Kata nne za Jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni Eng. Mpinga(Elerai) na katikati ni Malance Kinabo (Themi)

DSC06872Mgombea wa Chadema Kata ya Makuyuni (Monduli) Bw Japhet Sironga Lairumbe alitambulishwa mkutanoni hapo. Kesho Mei 19, 2012 uziduzi ramsi kwa Kata ya makuyuni kwa upande wa Chadema unatarajiwa kufanyika chini ya usimamizi wa Mh Godbless Lema ambaye ameahidi kutojerea Bungeni hadi ahakikishe ameacha Halmashauri ikiwa na wajumbe wengi zaidi wa Chadema.

DSC06874Mh Lema akimtambulisha mgombea wa Chadema Kata ya Kimandolu, Bw Rayson Ngowi

DSC06798Baadhi ya vijana waliojipamba kwa nakshi za rangi zinazotengeneza bendera ya Chadema, wakipozi viwanjani hapo. Kutoka kushoto Chris Nnko, Moses Joseph, Julieth William, Zion WIlliam na Nuru Ndosi

DSC06800“Bossi Mzito” wa ARUSHA255 akipozi kunukuliwa taswira viwanjani hapo akikusanya matukio.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO