Nyota wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas na Alex Song wakishangilia kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Barcelona
Wachezaji wa Barcelona wakishangilia taji la La Liga
Alexis Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya Lionel Messi kutoka
Radamel Falcao akishangilia bao lake
PAMOJA na kwamba Lionel Messi alishindwa kucheza jana kutokana na kusumbuliwa na maumivu, lakini haikuzuia Barcelona kushinda 2-1 dhidi ya Atletico Madrid usiku wa jana na kushangilia taji la 22 la Ligi Kuu Hispania.
Messi alianza katika mechi ya kwanza ndani ya raundi sita kwa sababu ya kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja la kulia, lakini akaondoka uwanjani dakika ya 68 Barcelona ikiwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Radamel Falcao dakika ya 52 na Barca ikakamilisha wachezaji wote watatu wa kubadilisha.
Hata hivyo, Alexis Sanchez akasawazisha dakika ya 72 na kiungo wa Atletico, Gabi Fernandez akajifunga dakika ya 80 hivyo kuamsha pati la ubingwa kwa Barcelona, wakiivua rasmi ubingwa Real Madrid.
Mapema siku hiyo, Valencia ilijiongezea matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Rayo Vallecano.
Roberto Soldado alifunga mabao mawili kabla ya mapumziko, wakati Andres Guardado na Nelson Valdez wakakamilisha karamu ya mabao kipindi cha pili.
Huo ulikuwa ushindi wa pili mfululizo wa 4-0 kwa Valencia na unamaanisha timu ya Ernesto Valverde inaizidi kwa pointi moja Real Sociedad, ambayo leo itakuwa mwenyeji wa Granada.
Malaga na Sevilla zote zina nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya baada ya sare ya bila kufungana uwanja wa La Rosaleda.
Stori na Picha kwa msaada wa Jackson Audiface Blog
0 maoni:
Post a Comment