Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Mkoani Arusha (Women Media Organization) wamefanya uchaguzi wa Taasisi hiyo na kuwachagua viongozi watakaowaongoza.
Katika uchaguzi huo uliofanyika Jumatatu Agosti 6, 2012 jijini Arusha Jamila Omary alifanikiwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho nafasi ya Makamu Mwenyekiti imechukuliwa na Mary Mwita na Ukatibu kwenda kwa Grace Macha vilevile katibu msaidizi aliyechaguliwa ni Ashura Mohamed
Viongozi wengine ni pamoja na mweka hazina wa chama Cynthia Mwilolezi na msaidizi wake ni Happy Lazaro, huku wajumbe wakamati hiyo ni pamoja na Pamela Mollel, Anjelina Karani, Rotlinde Philip.Veronica Mheta na Mwanaidi Mkwizu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho Jamila Omary alisema kuwa lengo la chama hicho ni kutetea na kupigania haki za wanahabari wanawake pamoja na kutumia fursa walizonazo katika kunufaisha jamii
Baadhi ya Viongozi walio chaguliwa wa chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake wa Mkoa wa Arusha , kulia ni mweka Hazina Cynthia Mwilolezi, katikati ni Mwenyekiti wa Chama Jamila Omary kushoto, ni Katibu Msaidizi Ashura Mohamed na nyuma ni Mjumbe wa kamati Pamela Mollel
Posted by Pamela Mollel on August 7, 2012
0 maoni:
Post a Comment