Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Magari yapinduka alfajiri ya leo Jijini Arusha

Kamera yetu imeweza kunasa tukio la ajali mbili za barabarani zikihusiha gari la abiria “kifodi” na gari ndogo “salon” kwatika maeneo tofauti ya Barabara ya Mandela kama picha zifuatavyo zinavyoonesha

SAM_3824Gari hili ambalo namba zake haizjaweza kupatikana mapema limekutwa na mpiga picha wetu asubuhi ya leo eneo ljinani na geti la kuingilia depot ya Coca Cola Kijenge Chini likiwa mtaroni pembezoni mwa huku eneo la mbele likiwa limeharibika vibaya. Haijaweza kufahamika chanzo cha ajli hiyo na hali za waliokuwamo garini wakati wa ajali.

SAM_3822

SAM_3821

SAM_3820

Tukio jingine ni la Hiace inayotoa huduma za kubeba abiria maarufu kama ‘Kifodi’ nalo likiwa limeharibika vibaya baada ya kuacha njia, kuparamia mti na kuingia korongoni. Ajali hii imetokea eneo lenye kona kali jirani na eneo maarufu kama Kona ya Banana-Kijenge. Haijaweza kufahamika pia chanzo cha ajali hiyo na hali za waliokuwamo. Matukio yote yamekutwa asubuhi ya leo.

Kwa siku nzima ya jana, Mji wa Arusha na viunga vyake ulikuwa na mfululizo wa mvua isiyokoma hadi usiku. Pengine hali ya utelezi na mwendo kasi wa madereva ukawa ndio sababu ya ajali hizi. Askari wa usalama barabarani walishafika maeneo hayo tayari kwa kazi yao. Blog hii itaendelea kufuatilia na kukujuza zaidi

MATUKIO MENGINE YA VIFODI KUANGUKA MWAKA HUU

ajali Kijenge (2)[4]

Hii ilitokea Mei 28, 2012 eneo la Kijenge mzunguko ikihusisha gari lenye usajili wa namba T481 AFS

kifodiNa hii ilitokea eneo la Moshono – Kwa Siara Julai 23, 2012 ikihusisha gari lenye usajili wa namba T621 AUF

Picha zote na Tumainiel W. Seria

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO