Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Waziri Mkuu Pinda Mgeni Rasmi Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini leo; maelfu ya watu wajitokeza siku ya kilele

SAM_3701

Waziri Mkuu, Mh Pindaoti la khaki katikati) akizuru banda la NMB katika siku ya kilele cha maonesho ya Nane nane Arusha mchana huu.

SAM_3700

SAM_3697

Wanausalama wakiwa makini kuhakikisha kuwa hakuna madhara yatakayomkuta kiongozi huyo Mkuu

 Waziri  Mkuu Mizengo Pinda akifurahia mzinga wa nyuki aliozawadiwa na TASO katika maonyesho ya Wakulima Nanenane kwenye uwanja wa Themi Arusha Agust 8,  2012.  Kulia ni Naibu Waziri wa Kiolimo na Chakula na Ushirika, Adam Malima

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akikagua mazao ya mbogamboga wakati alipotmbelea maonyesho ya wakulima  Nanenane kwenye uwanja vya Themi, Arusha Agust  8, 2012.

SAM_3685

Baadhi ya vikombe kwa ajili ya washindi mbalimbali wa maonesho haya Kanda ya Kaskazini

SAM_3724

Elimu ya kilimo cha mboga mboga – bustani mfano ikionesha sampuli za mboga na viungo tofauti tofauti

SAM_3723

Ufugaji wa kuku kisayansi

SAM_3720

Ng’ombe maksai

SAM_3721

Ukaushaji wa ngozi

SAM_3711

Zana za kilimo

SAM_3703

Makampuni ya huduma za mawasiliano nayo hayakuwa nyuma..

SAM_3708

Sunrise Redio ya Arusha nao walikuwepo wakirusha matangazo yao ‘live’ tokea viwanjani hapo

SAM_3687

Burudani za muziki live

SAM_3714

Banda la TAHA

SAM_3715

Huduma za ushauri nasaha na upimaji VVU

SAM_3694

Chuo cha Teknolojia Arusha kilikuwa na maonesho ya teknionlijia ya taa za kuongozea magari

SAM_3689

Ofisi ya TASO Kanad ya Kaskazini ambao ndio waandaaji wa maonesho haya

SAM_3692

Banda la Benki Kuu ya Tanzania

SAM_3691

SAM_3674

Misururu ya wananchi waliona shauku ya kuingia ndani.

SAM_3678

Msongamano wa watu ndani ya viwanja hivyo

SAM_3676

Kamera yetu pia ilimnasa raia huyu wa kigeni akiwa ametoka kufanya manunuzi ya mahitaji yake viwanjani humo

*****************

Waziri Mkuu, Mh M. Pinda amefanya ziara katika viwanja vya maonesho ya wakulima nchini maarufu kama ‘nane nane’ vilivyopo eneo la Njiro, Jijini Arusha, ambapo atahutubia maelfu ya wananchi wanaozidi kujongea vilivipo viwabja hivyo.

Kauli mbiu ya siku ya Wakulima “Nane Nane” kwa mwaka huu ni "KILIMO KWANZA ZALISHA KISAYANSI NA KITEKNOLOJIA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA ONGEZEKO LA IDADI YA WATU"

Kamera ya Blog hii ilifanikiwa kunasa matukio ya Waziri Mkuu akiwa katika banda la Benki ya NMB.

Mbali na hilo, kamera yetu iliweza kunasa misururu ya watu nje na ndani ya viwanja wote wakiwa na shauku ya kushiriki sherehe hizo. Vikundi mbalimbali vya burudani vipo vinatoa burudani.

Huduma na elimu za kiafya, kilimo, ufugaji, sayansi na teknolojia, sambamba na biashara ni baadhi ya shughuli zinaoelelea viwanjani humo chini ya uandaaji wa Chama cha Wakulima na Wafugaji Kanda ya kaskazini (TASO). Picha zote na Tumainiel W. Seria

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO