Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BAADA YA WATU KUKAIDI AGIZO LA WAZIRI MKUU, WANANCHI WACHOMA MOTO PAMPU ZA MAJI KARATU, MBUNGE NA MWENYEKITI HALMASHAURI WAKAMATWA NA POLISI

Vero Ignatus,Arusha 
Sakata la viongozi wa Chadema na wananchi wa vijijini nne wilayani Karatu Mkoani Arusha kukamatwa na polisi kwa kosa la kuchoma  mashine ya kuvutia maji ni kufuatia haa za baadhi ya watu kukaidi amri ya Waziri Mkuu aliyetaka mashine hizo zote kuondolewa katika chanzo cha maji kilichokuwa na mgogoro wa muda mrefu. 


Waziri Mkuu,Kassimu Majaliwa Mnamo desemba 5 mwaka huu,alimwagiza Mkuu wa wilaya ya Karatu, Theresia  Mahongo kuhakikisha kabla ya saa 12 jioni nay eye kumaliza kikao na wananchi awe ameziondoa mashine hizo zilizowekwa katika chanzo cha maji.



 
Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice aliyevaa kitenge akiwa na baadhi ya wananchi wa wilaya ya karatu leo katika kito cha polisi mjini kati Jijini Arusha.
Picha na Vero Ignatus blog.


 Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola, Maria Patrice





 
 Baadhi ya wananchi kutoka wilaya ya karatu wakiwa nje ya kituo cha polisi mjini kati leo.


***************
Mbali ya hilo Waziri  Mkuu aliagiza chanzo hicho cha maji kutunzwa na mashine zote ziwe umbali wa mita 500 na mto utunzwe kwa mita 60 tofauti na hapo hatua kali zichukuliwe.

Kufuatia agizo hilo vifaa hivyo na vingine viliondolewa vyote kwa kusimamiwa na Mkuu wa wilaya Karatu mwenyewe na jeshi la polisi wilaya ya Karatu.

Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice akizunzgumza na waandishi wa habari leo amesema kuwa baada ya agizo hilo kutekelezwa walirudi katika vikao vya jumuiya ya uongozi wa vijiji saba vya kata mbili za Mang’ola na Qaedenti kwa ajili ya kufanya maazimio ya agizo la Waziri Mkuu.

Amesema vijiji vyote viliafiki agizo hilo na kuahidi kutunza chanzo hicho cha maji umbali wa wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho na mita 60 kutoka kwenye mto.

Patrice ameendelea kueleza kuwa maazimio hayo yalikubaliwa na viongozi na wananchi wa vijiji vyote kwani kiliagizwa na Waziri Mkuu ni msisitizo kwani katika vikao vya nyuma vya vijiji hivyo hayo yote yalikubaliwa katika vikao.

Alisema cha kushangaza baadhi ya viongozi na madiwani kukamatwa kwani ndio waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanatii amri ya Waziri Mkuu.

Diwani huyo alisema kuwa aliambiwa kuwa baadhi ya wananchi wamerudisha mashine na vifaa vingine katika chanzo hicho cha maji na kufikia hatua ya wananchi wengine kukasirishwa na kitendio hicho cha kudharau mamlaka za juu zilizoagiza.

‘’Baadhi ya watu waliokamatwa hawahusiki kabisa na uchomwaji wa mashine hizo kwani polisi imeamua kukamata hovyo hovyo ila mie ninachojuwa desemba 26 na 27 mwaka huu baadhi ya wananchi walialikwa kufanya usafi katika chanzo hicho na kwa kuw amaji yalikuwa yakipungua siku hadi siku’’alisema diwani huyo

Mkazi mwingine wa Kata ya Mang’ola aliyeomba kutotajwa jina lake alisema kuwa mgogoro huo ni wa muda mrefu sana kutoka mwaka 2007 na kijiji cha Qaedenti ndio chanzo mgogoro huo kwani wamekuwa waghumu kutii maagizo ya viongozi wa juu wa serikali pindi wanapotakiwa kukaa umbali wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho cha maji.

‘’wamekuwa wakileta vurugu kila mara kwa sababu ya madai kuwa chanzo hicho ni chao lakini sio kweli kwani chanzo hicho hutoa huduma ya maji kwa vijiji saba bila ya kuwa na ubaguzi wowote’’alisema mwananchi huyo

Alisema kuchomwa kwa mashine ni kutokana na wananchi kupatwa na hasira na jazba za baadhi ya wananchi kurudisha mashine na vifaa vingine katika chanzo hicho cha maji na kudharau agizo la Waziri Mkuu.

Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Karatu ,Willy Qambalo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ,Jubillet Manyenyo wameachiwa kwa dhamana na wametakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi Arusha januari 4 mwakani.

Wengine waliokamatwa na bado wanahojiwa na polisi Arusha ni pamoja na diwani wa kata ya Baray ,Thomas Darabe na diwani wa kata ya Mang’ola Lazaro Emmanuel .

Kamata kamata hiyo imewakumba wananchi wengine ambao ni pamoja na Godwin Mussa,Safari Awak,George Pius,Baridi John,Bartazar Lohay,Jafari Thiophil,Vicent Airo ,sebastian Mosses na Daniel Ninida.

Wengine waliokamatwa na polisi ambao ni ndugu ni pamoja na ndugu wawili ambao ni pamoja na Charles Lameck na Chrisopher Lameck .

Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa baada ya kuchukuliwa maelezo kwa watuhumiwa hao 15 majalada yanapelekwa katika ofisi ya Mwansheria wa serikali kwa ajili ya kufungua kesi.

   
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO