Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

RIDHIWANI KIKWETE AAHIDI MSAADA KWA WASANNII KATIKA TUKIO LA UZINDUNI WA VIDEO YA BELLE 9"GIVE IT TO ME"


Mbunge wa Jimbo la Chalinze RIDHIWANI KIKWETE, amesema anataka kuona Wasanii Watanzania kazi zao zinatambuliwa na kuona faida ya kazi wanazofanya.
          Aidha amesema yeye kama Mbunge Kijana, anapenda kuona Wanamuziki wa Tanzania wakifanya vizuri na kuona faida ya kazi zao na kukuza soko la Muziki wao Kimataifa.
          Mbunge huyo amesema hayo alipokua Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Video ya mwanamuziki Belle 9 ya muziki wake mpya unaoitwa Give It To Me ambao amemshirikisha mwanamuziki G Nako.
          Akizungumza katika Uzinduzi huo, amesema anapenda kuona muziki wa Tanzania na wasanii wake kazi zao zikitambulika na pia waone faida ya kazi wanayoifanya.
          Katika Uzinduzi huo amesema amejitoa kumsaidia Msanii Belle 9 kutokana na uwezo wake wa Kuimba na kipaji alichonacho.
          Ameongeza kuwa yeye ni Mbunge kijana anayetaka kuona wasanii Watanzania kazi zao zinatambuliwa na kuona faida ya kazi wanazofanya.
          Aidha ameupongeza uongozi mzima wa Vitamin Music kwa kufanikisha tukio hilo na kusema wimbo wa Give It To Me bila shaka, unaongeza idadi ya nyimbo zitakazokuwa maarufu kwenye Klabu za Tanzania.
          Ameeleza kwamba anafurahi kuona wasanii wanaanza kuondoa ile imani kuwa Bongo Flava ni muziki wa kusikiliza zaidi, na kusema ndio maana unakuta hafla mbalimbali ikiwemo Harusi au mashindano kama Miss Tanzania, zinajaa Playlist za nyimbo za Nigeria.
          Aidha amepongeza Wanamuziki kwa hatua yao ya kufikiria kuweka ‘fusion’ za muziki wa Asili kwenye nyimbo zao ili kuzipa ‘Utanzania’ unaoliliwa kila siku.
          Amesema Wimbo huo wa Belle 9 una Video nzuri na anaamini itamfikisha Belle sehemu ambazo bado hajafika.

SOURCED FROM: LIBENEKE LA KASKAZINI

Msanii Bell 9 akipozi katika red carpet wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo wake wa Give It To Me.

Mgeni Rasmi katik uzinduzi huo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza katika uzinduzi huo.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO