Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Waziri Mkuu Majaliwa Azungumza na WafanyabiasharaArusha na Kuwaahidi Ushirikiano wa Serikali Kufungua Viwanda Zaidi

Mhe.Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wafanyabiashara wa Jiji la Arusha katika ukumbi wa AICC,Jijini Arusha.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Mjaliwa amewata wafanyabiashara kuwekeza zaidi kwenye sekta mbalimbali hasa za viwanda hapa nchini.

Aliyasema hayo alipokutana na wafanyabiashara wa jiji la Arusha nakuwashauri wawekeze kwenye mikoa yote ya Tanzania hasa kwakuanzisha viwanda,ilikujenga nchi ya viwanda kama dhamira ya serikali ilivyo.

“Nawashuri muwekeze kwenye mikoa yote hapa nchini na ni ruksa kabisa viwanda vingi vianzishwe”.

Hata hivyo amewata waendelee  kushirikiana na serikali yao ya awamu ya tano kwakuwa ipo pamoja nao na inaongeza ulinzi zaidi kwa wafanyakazi wote nchini ili wawe na amani na waweze kuwekeza zaidi.

Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuboresha zaidi kwenye sekta binafsi hasa kwakupambana na wasiolipa kodi ili walipe nakuweka usawa katika biashara na kukuza ushindaji wa biashara.

Aidha Majaliwa amewataka watendaji wa serikali kuvilinda viwanda vya ndani kwakuhamasisha matumizi ya rasilimali za ndani napia kuzipunguzia ushuru ili viwanda viweze kukuwa kwa kasi kama serikali inavyodhamiria kujenga nchi ya viwanda.

Majaliwa bado anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Arusha kwa kutembelea halmashauri zote za Mkoa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Lekule Laiza(kushoto)


Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO