Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mahakama Kuu Arusha ya tupilia mbali pingamizi la serikali dhidi ya maombi ya Lema kuongezewa muda wa kukata rufaa

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akizungumza na mkewe pamoja na wakili wake Sheck Mfinanga baada ya mahakama kumalizika. Picha na Vero Ignatus Blog.
Mbunge Godbless Lema akiwa na mahabusu wengine juzi baada ya kushuka kwenye gari la magereza. 

Na.Vero Ignatus Arusha.

  
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali dhidi ya maombi ya nyongeza ya muda kuwasilisha kusudio la kukataa rufaa ya kupinga dhamana ya mbunge Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lemakuhusiana na kesi ya uchochezi inayomkabili.

Jaji  Dkt.Modesta Opiyo wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha alisema katika maamuzi yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa mahakamani.

Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shedrack Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha hoja zao katika kiapo na hati ya dharura.

Akizungumza baada ya kukubaliwa na Jaji ,wakili Mfinanga alimtaka Jaji huyo kusikiliza rufaa hiyo kwani kuchelewa siyo sababu ya msingi sana kwa mujibu wa sheria na kunukuu kesi mbalimbali zilizochelewa kukatiwa rufaa kwa siku nyingi na kudai kuwa mahakama ya rufaa ilizikubali na kuzitolea maamuzi.

Mfinanga amesema na kumwomba Jaji kusikiliza rufaa yao kwa sababu ni ya msingi na kamwe haiwezi kuvunja sheria ya makosa ya jinai iliyowekwa kwa mujibu wa sheria.

Mawakili wa serikali wakiongozwa na Wakili Mfawidhi Materius Marandu, Hashim Ngole na Elizabert Swai walipinga vikali kukubaliwa kwa rufaa hiyo kwa madai kuwa Jaji Msengi alitupilia mbali na kurudia kuikubali ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za makosa ya Jinai.

Baada ya malumbano hayo yaliyochukuwa zaidi ya masaa 5  Jaji Opiyo alisema kuwa uamuzi wa kuikubali ama kuikataa rufaa hiyo atautoa kesho Desemba 20 mwaka huu majira ya saa 6 mchana katika mahakama hiyo.

Mbunge Godbless Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi aliyosomewa katika mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka huu Mkoani Dodoama kwa kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika kata mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi kwa wananchi waliomchagua kuwa Rais wa nchi.

CHANZO: VERO IGNATUS
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO