Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akiteta jambo na mke wake Neema Lema Tarimo katika chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Arusha jana. Picha na Vero Ignatus Blog. |
Arusha
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Dkt.Modesta Opiyo amempa siku kumi(10) Mbunge Godbless Lema kupitia mawakili wake wawe wamewasilisha notisi ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliyomnyima dhamana kwa kosa la uchochezi.
Agizo hilo limekuja kutokana na mahamama kutoridhishwa na hoja za maombi ya mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali dhidi ya taarifa ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa mbunge huyo

Jaji Dkt.Modesta Opiyo wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha alisema katika maamuzi yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa mahakamani, ambapo amesema mahakama haijaona ucheleweshwaji wa lazima.
Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shekh Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha notisi ndani ya siku kumi kuanzia jana, hadi hapo tar 30 Disemba 2016 shauri hilo litakaposikilizwa tena.

0 maoni:
Post a Comment