Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

James Millya Aongoza Zoezi la BAVICHA Arusha Kuchangia Damu Kwa Hiyari Hospitali ya Mt Meru

Mbunge wa Jimbo la Simanjiro kupitia CHADEMA, Mh James Ole Millya hii leo  ameongoza makumi ya vijana wa chama hicho waliojitokeza katika Hospitali ya Mt Meru kwa ajili ya kuchangia damu  kama sehemu ya mchango wao kwa jamii katika kukamilisha mwaka unaoelekea ukingoni.

Mratibu wa zoezi hilo ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Vijana CADEMA Wilaya ya Arusha Mjini ambaye pia niDiwani wa Viti Maalumu wa chama hicho Kata ya Levolosi Jijini hapa, Mh Glory Kaaya ameieleza blogu hii kuwa kama viongozi wa baraza walipata wazo la kuwakutanisha vijana wenzao na wanajamii wengine bila kujali itikadiza kisiasa kuweza kutoa mchango kwa jamii kaama sehemu ya shamrashamra za kumalizia mwaka 2016 na kwasababu walipata taarifa ya uhitaji mkubwa wa damu hopitalini hapo wakaona ni vyema wakajihamasisha na kusaidia kuchagia damu.

Zoezi bado linaendele na pindi likikamilika tutakufahamisha ni damukiasiganiimepatikana na ni watu wangapi wamejitolea pia. Tembelea tena ukurasa huu.. 

Mbunge James Millya akiendelea na zoezi la utoaji damu 

Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakijaza fomu maalumu kabla ya kufanyika kwa uchangiaji wa damuKatibu wa BAVICHA Arusha Mjini Mh Glory Kaaya akitolewa damu kuchangia wenye uhitaji katikahopsitali ya Mt Meru ya Jijini Arusha mapema asubuhi hii leo

Mh James Millya akiwa na baadhi ya viongozi wa BAVICHA Arusha Mjini katika Hopsitali ya Mt Meru
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO