Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbunge Cecilia Paresso apata ajali ya gari akitokea Arusha kurudi Karatu usiku.

Nanja, Arusha.
Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mh Cecilia Pareso na baadhiya madiwani wa Karatu wamenusurika katika ajali mbaya ya gari usiku huu eneo la Nanja wakitokea Arusha.

Katika gari hiyo, inaelezwa kuwa ilikuwa na jumla ya madiwani watano na mbunge Paresso wakitokea Arusha mjini kuwadhamini madiwani wenzao waliokamatwa katika kufuatia ziara ya RC Gambo Wilayani Karatu kufuatiliana mgogoro wa maji ambapo wananchi walichoma moto pampu za maji za wahusika waliokaidi amri ya waziri Mkuu kuwa papmu zote ziondolewe na zifungwe umbali wa mita 500 kutoka kwenye chanzo cha maji.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imetokea eneo la Nanja baada ya lori lililokuwa limeharibika na kupaki pembeni kutokuweka alama za  tahadhari na gari la mbunge kugonga lori hilo kwa nyuma. Hakuna aliyepata majeruha makubwa na wote wako hospitali ya Selian kwa uangalizi, isipokuwa tu gari limeharibika vibaya.
Namna gari ya Mbunge Paresso ilivyoharibika baada ya ajali
Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA Cecilia Paresso (aliyekiziba uso) akiwa katika Hopitali ya Seiliani ya Jijini Arusha baada ya ajali eneo la Nanja akirejea Karatu kutokea Arusha Mjini

Gari ya Mbunge Paresso ikiwa imeligonga lori liiloharibika barabarani usiku bila kuwa na viashiria vya kuharibikaWashirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO