Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAAMUZI YA RUFAA YA KESI YA LEMA KUJULIKANA JANUARI 4, 2017



Na.Vero Ignatus Arusha.

Mahakama kuu kanda ya Arusha imesikiliza maombi ya rufaa yayaliyowasilishwa na upande wa jamhuri na ule wa mshtakiwa Godbless Lema ambapo pande zote mbili wamekubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa jamhuri ambapo upande wa serikali wameiomba mahakama kuwasilisha kwa hati ya maandishi hapo keshokutwa tarehe 30 Disemba 2016

Aidha rufaa hizo ni pamoja na ile ya upande wa Jamhuri kutoridhika na maauzi ya Jaji Dkt. Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi (10) upande wa mshtakiwa Lema kufaili notisi ya rufaa ,na upande wa wamshtakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa lema masharti ya dhamana

Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 disemba 2016 ambapo tarehe 2 januari watakutana pande zote kwaajili ya kufanya majumuisho na maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 januari 2017

Hata hivyo baada ya kusikiliza rufaa hizo mahakama imeibua hoja yenyewe na kuwapa kazi mawakili wa pande zote mbili kuangalia kuwa notisi iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi matakwa ya kisheria?

Kwa upande wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala amesema kuwa kwa upande wao wameiomba mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza rufaa ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea sehemu moja  

"Unajua leo rufaa mbili zimegongana ile ya upande wa jamhuri na ile ya kwetu sisi,hivyo basi sisis tumeiomba mahakama kusitisha rufaa yetui isikilizwe ile ya serikali kwanza,kwani rufaa zote zinaelekea upandemmoja ,wandege apande ndege na wa basi apande basi "alisema Kibatala.

Hata hivyo mbunge huyo wa Arusha mjini Godbless lema amerudishwa rumande hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na mahakama.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO