Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TAARIFA KUTOKA CHADEMA KANDA YA KASKAZINI KUHUSU MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA MARUDIO KATA NNE

*MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA MARUDIO YA KATA NNE KASKAZINI.*

Ofisi ya katibu wa Kanda ya Kaskazini leo imepokea Mchango wa chakula kutoka kwa Baraza la vijana wa Chadema Mkoa wa Arusha (BAVICHA) kwa ajili yakusaidia timu za makamanda zitakazokua FIELD (NGOME) wakati wa Kampeni.

Bavicha Mkoa wa Arusha wametoa Chakula kwa ajili ya Kata ya Lembeni Jimbo la Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Vitu vilivyotolewa ni pamoja na Mafuta ya kupikia Lita 10 Mchele Kilo 25 Maharage Kilo 20, Unga Kilo 20,Sukari Kilo15, Majani ya Chai pamoja na Chumvi, sambamba na kuahidi kuhamasishana vijana kujitokeza na kwenda kushiriki FIELD kwenye kampeni kwa kipindi chote.

PICHANI:Katibu wa kanda ya kaskazini na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha Mhe.Amani Golugwa akipokea vitu hivyo kutoka kwa Jenipher Mwasha Katibu wa Bavicha Mkoa wa Arusha.

Mhe.Amani Golugwa aliwashukuru na kuwapongeza Bavicha Mkoa wa Arusha kwa kitendo hicho hasa kutoa na kuelekeza vitu hivyo vipelekwe nje ya Mkoa wao.
Aliwaomba wana CHADEMA wengine kujitokeza na kuchangia kampeni hizi ambapo Chama kimedhamiria kushinda.
Katibu wa kanda alimalizia kwa kusema kwenye uchaguzi huu "It is We Either Win Or they Loose"

Kata ambazo uchaguzi unarudiwa ni; Lembeni (Mwanga), Mateves (Arumeru Magharibi), Ngarenanyuki (Arumeru Mashariki) na Duru (Babati Vijijini). Kampeni zitaanza tarehe 23 Desemba 2016 hadi 21 Januari 2017 na uchaguzi kufanyika tarehe 22 Januari 2017.

Imetolewa na
Mozec Joseph
Afisa habari- CHADEMA Kanda ya kaskazini.
15/12/2016

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO