Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAJIPANGA KUJENGA 'MACHINGA COMPLEX' JIRANI NA KILOMBERO SOKONI

Na.Vero Ignatus ,Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha limeanza utekelezaji wa Agizo la Rais
John Pombe Magufuli la kuwatafutia wafanya biashara wadogo ‘machinga’
eneo salama kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.

Katika utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli, sambamba na kuondoa
kero hiyo, uongozi wa Jiji la Arusha umenza hatua za awali za kujenga
jengo la kufanyia shughuli wafanyabiashara wadogo maarufu kama
‘Wamachinga complex.

Mradi huo unaolengwa kufanyika katika eneo lililopo mkabala na soko la
kilombero kiwanja Namba 69 chenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja,
lililorejeshwa hivi karibuni serikalini na waziri mkuu, Kasim Majaliwa
wakati wa ziara yake mkoani Arusha.

Akiliongelea suala hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,
Athumani Kihamia alisema eneo hilo lina uwezo wa kuhifadhi
wafanyabiashara wadogo zaidi ya 2000 pamoja na shughuli zao mara baada
ya mradi wa kujenga miundombinu utakapokamilika.

“Baada ya agizo la Rais na kero inayojitokeza tumeamua kufanya haraka
zaidi ambapo hadi jana tumeshaunda kamati inayofanya tathmini ya
ujenzi wa eneo hilo, na lengo ni kuakikisha tutawaondoa
wafanyabiashara kutoka kwenye maeneo hatarishi ambayo wengi ndio
wanayatumia kufanya shughuli zao, hii ni pamoja na kando za barabara
ya Maromboso, stendi kuu na ile ya Col. Middleton,” alisema Kihamia

“Pamoja na kuwa katika uongozi wa jiji ukiwaandalia maeneo mengine ya
kufanyia biashara zao, ni vizuri wafanyabiashara hawa waendeleze
shughuli kwa busara bila kuvunja sheria, hususan za barabarani au
kuvamia sehemu za maduka na biashara za watu wengine, ikiwemo kujali
usalama wao binafsi,maana sasa wamefunga hata badhi ya barabara,”
alisema Kihamia.

Mmoja wa wafanyabiashara wadogo anayeuza viatu, Hussein Issa, ameomba
kusiwepo na urasimu wakati wa ugawaji wa maeneo ya biashara
yaliyotengwa; “tatizo wala sio wingi wa wamachinga, bali ni kwamba
vingozi wakubwa huwa wanahodhi maeneo hayo ili baadae waje kuwauzia
watu wengine, sasa unakuta mtu anamiliki maeneo zaidi ya kumi peke
yake ili ayauze au awakodishie watu,” alisema.
Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO