Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Ziara ya Kikazi ya Waziri Mkuu Majaliwa Wilaya ya Karatu


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akisoma mabango ya wananchi wa kijiji cha Qandged wilayani Karatu baada yakufunga njia kuzuia msafara wake usipite.

Picha ya pili
Kassim Majaliwa akikagua mfereji wa maji uliojengwa na World Vision unaopeleka maji kwenye kisima katika kijiji cha Jobaj.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo kuondoa mashine zakupampu maji zilizowekwa kwenye chanzo cha maji cha kijiji cha Qangded kata ya Eyasi wilayani Karatu.

Akitoa maelekezo hayo Majaliwa wakati  alipokuwa anaongea na wanakijiji wa Jobaj katika mkutano wa hadhara ambapo alizindua kisima cha maji.

Alisema mashine hizo zimekuwa zikitumika kunyeshea mashamba ya wafanyabiashara  wakubwa wa vitunguu na mahindi nakusababisha kasi ya maji kwenye mifereji kupungua nakupelekea wakazi wengi wa kijiji hicho kukosa maji kwa mda mrefu.

“Baada ya siku moja Mkuu wa wilaya apite kukagua na akikuta bado mashine hizo zipo azikamate nakuwachukulia hatua kali wahusika kwakuwa wanaharibu vyanzo vya maji”. Alisema.

Pia amewataka wananchi wote kuwa walinzi wa vyanzo vya maji vilivyopo katika maeneo yao na watoe taarifa mapema kwa mamlaka husika pale wanapogundua kuna uharibifu umefanyika.

Wananchi wanatakiwa kufuata sheria yakutofanya shughuli zozote za uzalishaji ndani ya mita 500 kutoka katika vyanzo vya maji na waliofanya hivyo waondolewe mara moja.

Majaliwa amelipongeza shirika la World Vision Karatu kwakujenga mifereji yakutoa maji kwenye chanzo  cha maji hadi kwenye visima ambavyo wananchi wanapata maji,hizo ni juhudi kubwa zilizofanywa na shirika hilo na serikali inatambua mchango wao huo mkubwa.

Amewata mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri kujenga utamaduni wakusiliza kero mbalimbali za wananchi nakuzichukulia hatua mara moja.

Picha ya tatu.
Majaliwa akikagua moja ya shamba lililolimwa kutokana na kilimo cha umwagiliaji cha kijiji cha Qandged wilayani Karatu.

Picha ya nne
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia kwake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakikata utepe kama ishara yauzinduzi wa kisima cha maji cha kijiji cha Jobaj wilayani Karatu.

Picha ya tano
Waziri Mkuu Kassim Mjaliwa(MB) akuzungumza na wananchi wa Karatu katika uwanja wa Baraa Karatu Mjini baada yakumaliza ziara wilayani humo.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO